Tujadili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Oct 26, 2010.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hivi ingekuwa wewe umekumbana na hii kitu ungefanyaje?
  Nimeisoma hii nimeona niilete huku tuijadili! Iwapo utamkuta mwanao wa kiume au wa kike na hii kitu utachukua hatua gani?

  MWANAMKE mmoja [49] mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam, jana nusura aue mtoto wa kumzaa mwenyewe kwa kumkuta na ganda la mpira wa kiume “ Kondom” kwenye mfuko wa madaftari wakati alipokuwa akikagua madaftari yake
  Mwanamke huyo alimuamuru mwanae huyo wa kiume asomae kidato cha pili amletee madaftari yake ili aweze kukagua alichokisoma kwa kipindi cha wiki nzima na kukutana na dhahama hiyo ambayo hakuitarajia machoni mwake .

  Ilidaiwa kuwa, mwanamke huyo mfanyakazi wa Tanesco alichukua daftari hizo na kuingia nazo chumbani kwake na kuanza ukaguzi juu ya madaftari hayo na ilidaiwa wakati akiwa mwishoni wa ukaguzi huo aliona ganda hilo lililoanguka kutokea kwenye mifuko ya pembezoni mwa mfuko yalimokuwa madaftari hayo.

  Ilidaiwa hakuamini macho yake kwanza kwa kuwa aina hiyo ya mpira hakuwahi kuiona wala kuisikia na alimuita mdogo wake mmoja wa kike aliyekuja kumtembelea hapo wiki moja nyuma alimuonbyesha ganda hilo na kumuuliza ni la nini na alimbainishia kuwa ni ganda la kondom na mama huyo ilidaiwa jasho jembamba lilianza kumchuruzika na kuanza kulia akiwa chumbani kwake.

  Ndipo alipomaliza kulia na kuona amepata nafuu alimuamuru mdogo wake huyo amuite mwanae huyo na alipoingia humo hakutaka kumuuliza swali lolote na alianza kwa kumpa kichapo bila mtoto huyo kutambua alikuwa na kosa gani.

  Ilidaiwa kuwa, mdogo wake pamoja na msichana wa kazi waliingia chumbani humo kumuamuru aache kumchapa lakini juhudi zao hazikuzaa matunda na mtoto huyo kupiga kelele kutokana kipigo hicho, ndipo walipoamua wafungue geti kuomba msaada kwa jirani yao wa karibu ili akamwambie aache kumuadhibu kijana huyo.

  Juhudi hizo ndizo zilizaa matunda na kwa heshima ya jirani yake huyo ndio mama huyo alikubali kumuaacha kumpiga mtoto huyo kwa kutumia mkanda wa suruali na fimbo ya fagio wa wima wa kufagilia ndani.

  Hata hivyo ilidaiwa baada ya kumaliza kipigo hicho mtotto huyo alikuwa amechoka sana kwa kipigo hicho na aliweza kumjeruhi kidogo, mwanamke huyo aliwasha gari na kumkimbiza mwanae huyo hospitalini kwa matibabu.

  Hata hivyo nifahamishe ilibahatika kuonana na mwanamke huyo siku iliyofuata na hakuwa tayari kuongelea suala hilo ka kuhofia kunukuliwa huku akiomba asirushwe kwenye mtandao huu.

  “Ujue nilikuwa na hasira sana, umri huu, nimemkuta na ………., yesu wangu, Mungu anisamehe, inamana ameshaanza……, nitamuombea, ujue ukishamuacha mtoto hivyo atajua ni kawaida, mimi sikumuuliza lolote, mimi nimejua tu alitumia yeye
   
 2. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mama wengine jamani, hakutenda haki kumpiga mtoto huyo!
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kibweka naona umeamua kutukimbiza duh hata hatujui turespond kwenye mada gani. Na uzee huu hizi mbio zitatuua.

  Hii inaonyesha jinsi gani campaign ya Break the ice haijafanya kazi. Kama mama huyu angekuwa amevunja ukimya siku nyingi na wanae wala hili lisingemshangaza. Tatizo letu wazazi hasa kina mama huwa hatutaki kukubali kuwa wanetu wanakua kwa kazi tofauti na ile tuliyokulia sisi, kila siku tunawaona bado wadogo matokeo yake tunapata presha pale tunapojikuta tunakumbana na mimba za utotoni kwa watoto wetu na kuishia kujuta.
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wewe ungefanyaje MOM?
  Mie ningetoka tratiibu kwenda pata mbili tatu baridi moto narudi najadiliana kwanza na wife hiyo kitu
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ngoja nipunguze kuwatoa NYUTI.....Ila haya tunakumbana nayo Wajameni tupeane mauzoefu ya slove ma problemaaa
   
 6. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ningetafakari kwanza, sipendi kuruhusu hasira zinitawale. then nipange jinsi ya kuongea na mtoto wangu A-Z ya mapenzi katika umri mdogo, na umuhimu wa kutumia kile alichokuwa nacho kwenye daftari. sasa huyu alivyompiga mtoto ukute hata hajawahi kutumia hiyo kitu wala kuwa na mpenzi amemjengea mtoto picha gani? yani ameshajenga uadui na mtoto wake
   
 7. T

  The King JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mama kakurupuka kwa kuamua kumpa kichapo mwanae. Angemkanya tu kwamba mwanaye huyo bado mdogo kujihusisha na mambo ya kujamiiana. Na kuanza kumfuatilia kwa karibu mno nyendo zake za kila siku.
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sasa huyu mama alichoshangaa ni nini?alitaka mtoto wake afanye mapenzi pimbina?hiyo ilikuwa ni ishara njema ya kuwa mtoto yupo salama kwa kuwa anajikinga na magonjwa!
   
 9. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Masamiati mkuu! Fafanua hapo
   
 10. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huyu mama alihitaji muda wa kutulia na kutafakari kama MOM alivyosema,angeongea na mtoto angepata ukweli wenyewe then angejua pa kuanzia.
   
Loading...