TUJADILI: Tabia ya watu kuacha miswaki chooni na bafuni

TUJADILI: Tabia ya watu kuacha miswaki chooni na bafuni

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
17,306
Reaction score
19,880
images.jpeg


Wakuu, habari za wakati huu. Bila shaka wote mu wazima na mnaendelea na shughuli za ujenzi wa taifa.

Wakuu, hivi hii tabia ya baadhi ya watu kupenda kuacha miswaki yao kwenye vyoo ama mabafu yanayotumiwa na wengi, ni ustaarabu kweli huu wakuu?

Unakuta nyumba ni self contained, ndani kuna vyumba vinne vya kulala, wanaishi watu kama 8 ama 9, they all share the same bathroom and toilet lakini ukienda unakutana na miswaki ya watu.

Unamuamini vipi mwenzako anayeingia kule bafuni ama chooni? Unajua anafanya nini na ile miswaki kwa bahati mbaya ama makusudi?

Hii tabia imeshamiri sana katika kaya nyingi sana amabazo nimewahi kuishi (ndugu, jamaa na marafiki) ndio maana nikaona ni vyema nilete hii suala hapa wakuu tulijadili sote kwa pamoja.

Hili jambo ni sahihi ama si sahihi wakuu?

WENGI WENYE TABIA HII WATASOMA BILA KUWEKA COMMENTS ZAO HAPA
 
Kwani vepe ata nguao chooni tutaanika
 
Mswaki usipokuwa bafuni utauweka wapi? Na kama ni self contained ina maana kila chumba kina bafu/ choo chake, tatizo liko wapi?
 
ile miswaki wala sio .. mie niliwahi kuishi kwa ndugu ambao huu uzungu uliwakolea ila ilinishinda wangu nilikuwa nainia nao room nauhifadhi kwenye begi, ile kuweka pale maranyingi huwa inadondoka mpka inazama kwenye tundu tunaitoa na kuimwagia maji na kuirudisha kwenye kikopo atajuaje akiingia atatumia ktu
 
Back
Top Bottom