serikali imehamia tunduru,operesheni ya kusaka majangiri na watu wanaojishughulisha na biashara ya nyara na uwindaji haramu imeshika kasi na kupelekea wananchi wengi kukimbia maeneo haya.hadi sasa watu wengi wanashikiliwa kwa mahojiano,baadhi wameshafikishwa mahakamani na wengine wameshahukumiwa.jambo la kustaajabisha ni kwamba watumishi wa serikali ambao wamekuwa kuchocheo kikubwa ktk shughuli hizi za ujangiri kwa kufadhili ama kushiriki wakiwemo maafisa maliasili wenyewe hakuna yeyote miongoni mwao ambae ameshakamatwa hadi sasa tangu operesheni hii ianze mwezi mmoja uliopita.hali hii inatuhuzunisha sana wananchi hasa ktk kuona serikali inakuwa makini na kutumia nguvu kubwa inaposhughulikia masuala yanayohusu wananchi wanyonge wa kada ya chini kabisa huku mafisadi na wenye nacho wakipeta tu bila kuguswa,je ni kutimiza maandiko kwamba alienacho ataongezewa na asienacho atanyang'anywa hata alichonacho?
Karibuni