Tujadili maendeleo ya Mtwara na Lindi

Tujadili maendeleo ya Mtwara na Lindi

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,315
wakuu salaam sana,
kwa walioko mtwara poleni sana kwa kutetea maslai yenu.
wakuu naomba sasa kuuliza maendeleo ya jumla kwa mikoa ya LINDI NA MTWARA
nataka nijue kama kuna barabara za lami km ngapi,huduma za maji,hospital na huduma zingine za kijamii.
mimi sijawahi kufika huko na ninaishi kanda ya ziwa na habari tunazozipata huku ni kuwa hiyo mikoa ni maskini wa kutupwa .
hata picha ninazoziona jf sijaona nyumba ya maana wala lami.
mods naombeni huu ukae hapa nipate majibu.
 
Lami
  • Dar_lindi _mtwara kuna lami
  • Lindi masasi kuna lami
  • barabara kuu za ndani ya lindi zina lami
  • Barabara kuu za mjini mtwara zina lami
Makazi
  • makazi ya wenyeji yanajengwa kwa kutumia nguzo za miti na kuezekwa kwa makuti, nadhani hiyo ni tamaduni ya ujenzi wao(by the way nguzo za kujengea ni nyingi)
  • Nyumba bora na za kisasa sana zimeanza kujitokeza katika maeneo ya mijini(Lindi, mnazi mmoja, Mtama, Nyangao, Masasi, Ruangwa, Mtwara
Umeme
  • Upo umeme utokanao na mitambo ya gesi
Maji
  • hali ya upatikanaji wa maji sio nzuri
Chakula
  • Chakula kinapatikana, mahindi na mchele (sio sana) lakini ipo mihogo, mbaazi na kunde za kutosha
Elimu
  • shule zipo za kutosha ila waalimu hawatoshi(utakumbuka kuna baadhi ya maeneo kama vile newala na tandahimba waalimu walichapwa viboko na wazazi wakati wa fujo za korosho) waalimu walikimbilia maeneo mengine

Comparison
ukikompea mkoa wa mtwara na mikoa kama tabora, kigoma na rukwa utaona kuwa mtwara iko better off(my opinion and i stand to be corrected)
 
Alichoongea Sendoro Mbuzi hapo juu ni sahihi Mtwara iko mbele kiasi fulani kimaendeleo kulinganisha na mikoa mingi ya kitanzania
 
Kwanini bandari ijengwe bagamoyo badala ya mtwara?

bandar inajengwa bagamoyo ili kuipunguzia uzito bandar ya dsm na kwa nn isiwe sehem nyingine ni kwamba bagamoyo ni karibu na dsm isitoshe nchi nying huptsha mizigo yao kupitia bandar ya dsm sasa ili kuipunguzia mzgo wameamua kujenga nyingine jirani ambapo ni bwagamoyo
 
Mtwara na lindi, mtwara ni afadhali kidogo kimaendeleo, kuna barabara mjini, lakini vijijini bado mambo sio mazuri! Lakini ni vizuri issue ya gesi ikaangaliwa kwa mapana yake!
 
Back
Top Bottom