Tujadili kuhusu "VAT"

Kwa kuongezea, VAT ni Added Value Tax kwa maana kuwa. Kuna TAX ya kawaida na VAT.
Mfano TAX ya kawaida 5% ya unga wa sembe ulio dukani na VAT 10%.
Sasa tuseme dukani umeenda kununua kila 10 kwa sh 1000 na Hapo dukani ndo kwa mara ya kwanza unga umeingia sokoni. Basi,TAX ya mwanzo mwenye duka analipa 10%X1000 , ambayo ni sawa ni sh 100.

Sasa Na wewe unaenda tena kuuza huu unga gulioni kwa sh 1500. Hapo umeongeza sh 500 ya bei ya awali, hiki ulichokiongza ndo kinaitwa ADDED VALUE. Na added Value hapo ni sh 500 na hivyo utalipa VAT ya 500 X10% sawa na sh50. Hii sh 50 ndo VAT maana umeongeza bei na ongezeko la bei kutoa ile principal ndo VAT.
 
 
Umejitahidi kufafanua mkuu hata hivyo mfanyabiashara anayekuuzia mzigo huwa bei yake ya mwisho tayari INA VAT ndio maana wewe unaona hujachajiwa kumbe kiuhalisia umechajiwa. Ndio maana ukienda dukani kariakoo kununua bidhaa wanakupa bei mbili, yenye. VAT na isiyo na vat. Utakuta wanakuuliza kama unataka risiti bei ni hii na bila risiti bei inakuwa chini. Ki msingi anayekuuzia mzigo au huduma ni Wakala wa TRA katika kukusanya vat mkuu.
 
Peleka p

Peleka pumba zako Lumumba.

Mlijifungia BUNGE la katika mkaja na katiba ya hovyo.
Mmejifungia BUNGE la bajeti mmekuja na bajeti ya hovyo.
 
Umeeleza vyema kama hawataki kuelewa basi waache waendelee kukamuliwa ili mradi serikali inapata 18%.
 
Mtoa mada ungekuwa darasani unge-score 70%, inaelekea hujui practicability yake. kuna kitu kinakutatiza nikipata muda nitakusaidia
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi. I concur with you 100%
 
UMEPAMBANUA vizuri sana swala la tax...ila kwangu mimi navyojua ndio maana utakuta katika kila mkoa kuna mageti ambayo yanazuia mazao kutoka na lazima kulipia..huyu mkulima wa maembe kama ataweza kula yote hawezi kulipa tax lakini kama akiuza haya maembe mnunuzi lazima akalipie TAX unless kama atauza kidogo kidogo lakini kama akiuza kama fuso must kulipia...kwenye point ambazo zipo barabarani na anapewa risiti.
1)VAT...value added tax....vat inalipwa na anayenunua bidhaa ila muuzaji anaisaidia serikali kukusanya ile kodi...mark up price lazima iwe zaidi ya tax ili nayeye apate faida na VAT ya TRA

2)bakhresa kuuza bidhaa yake lazima aangalie haya maembe aliyonunua amelipia sh ngapi, production cost,usafirishaji na anaweja mark up price ili apate faida pia

3) bidhaa zinaweza panda bei kutokana na costs ya vitu vingine zaidi ya VAT...mafuta,usafirishaji na production costs kitu ambacho upandisha bidhaa bei juu na ndipo muuzajia anapopandisha bei juu pia.
 
Mtoa mada tafadhali usipotoshe umma wa watanzania. Biblia inasema tafuta ukweli utakuweka huru. Naomba watanzania wenzangu kabla ya ku comment na kushukuru tufanye utafiti angalau kidogo ili kupanua ufahamu wetu wa mambo na kukwepa upotoshaji. VAT ni kodi ya ongezeko la thamani na kamwe hailipwi na mfanyabiashara ila mnunuzi. Swali linaweza kuja mbona kuna wafanyabiashara wananua bidhaa zinazotozwa VAT ni vipi hawailipi? Kama hawalipi VAT ni nani hasa analipa? Inatokea nini mpaka mfanyabiashara anaidai serikali arudishiwe VAT aliyolipa?

Ili tuelewe nitaleta mfano rahisi unaowahusisha wafanyabiashara wawili ambao wasajiliwa kutoza VAT. Mfanyabiashara akinunua bidhaa kwa mfanyabiasha mwingine ambayo bei tuchukulie bei ya bidhaa ni tshs 2,000 bila vat. Kwakuwa mfanyabiashara wa amesajiliwa kutoza vat ataongeza asilimia 18 kwenye bei aliyopanga na hivyo bei ya bidhaa hiyo itakuwa Tshs 2,360 kwa maana ya bei ya muuzaji tshs 2,000 + 18% ya tshs 2,000 ambayo ni tshs 360. Kama nilivyosema awali huyu aliyenunua pia anaenda kuuza. Bei yake ya kuuza ni tshs 3,000 bila vat yaani ameweka margin ya tshs 1,000. Sasa bei ya kuuza itakuwa tshs 3,540 yaani bei yake ya tshs 3,000 + 18% ya vat ambayo inatozwa kwenye tshs 3,000 bei ya muuzaji.

Sasa kwanini mfanyabiashara halipi vat? Kila mwisho wa mwezi mfanyabiashara aliyesajiliwa anatakiwa kupeleka return au repoti ya kodi ya vataliyokusanya. Mfanyabiashara huyu ataonyesha kodi aliyokusanya ni tshs 540 wakati huohuo ataonyesha kodi aliyolipa ya vat ya tshs 360. Kwakuwa alichokusanya ni kingi kuliko alicholipa basi tofauti ambayo ni tshs 180 atailipa tra. Kama alichokusanya ni kidogo kuliko alicholipa tra itatakiwa kumrudishia mfanyabiashara hicho alicholipa zaidi. Kwa mfano huu mfupi mtakuwa mmepata mwanga kwamba kodi hii inalipwa na mlaji wa mwisho.
 
Kwa mawazo yangu finyu kwenye mambo ya kifedha, natabiri mabenki yatapandisha gharama za huduma zake ili kufidia makato ya kodi. wakilazimishwa lazima watatoa sababu ya kupandisha bei ya huduma kwa maelezo ya kuweza kujiendesha. WATEJA KAMWE HATUTAEPUKA KUUBEBA MSALABA HUU!
 
Wewe ndiye unayepotosha. Kama huelewi it's better ukakaa kimya.
 
Usomi wako unanitia shaka, au labda tuseme mambo ya kodi sio fani yako, umeongea tu kama mtanzania wa kawaida, sasa kosa lako ni kuwa unataka kufundisha na wewe huyajui hayo mambo so unaishia kupotosha. siku nyingine fanya karesearch kidogo kwanza.
 
Usomi wako unanitia shaka, au labda tuseme mambo ya kodi sio fani yako, umeongea tu kama mtanzania wa kawaida, sasa kosa lako ni kuwa unataka kufundisha na wewe huyajui hayo mambo so unaishia kupotosha. siku nyingine fanya karesearch kidogo kwanza.
Sasa wewe uliyeelewa utuambie kama huu mfumo ni rafiki kwa maendeleo ya taifa letu na kwa raia.......maana wasomi wa tanzania huwa mnasahau kitu kimoja hii elimu ni ya mkoloni.......na alikuwa anaitumia kumnyonya raia mzawa leo tumerithi bado mnaona ni ujanja........kwa kifupi ukisha maliza degree yako unajiona mzungu ili hali ni mtu mweusi hadi unyayo.....

Soma vizur uelewe hoja niliyoleta sio unaruka tiki taka kwenye sakafu yenye utelezi utatulia kisogo uumie.....

Na hii mifumo ya kurithi haiishii kwenye kodi tu hata kwenye ulinzi na usalama mtaona mambo ni yale yale......askari anapewa mafunzo ya ukatili dhidi ya raia sio mafunzo ya kumtetea ...kumlinda....na kumuelekeza raia ...ila ni kumkung'uta kama ngoma iwe kwa kosa dogo au kubwa........na bado ukikosoa bado watakuja wanaojua zaidi watakwambia hapana askari wanavyofanya ni sahihi hapa nchini......

Inaboa sana watu mnavyeti halafu vimewavimbisha akili tu na manotes ya kumeza na hamjajifunza ili kuibadili direction nchi yetu iende kuzuri........tumia jicho la tatu
 
Mleta maada unaposha umma. kwanza unaonekana kujaisoma hiyo sheria ya kodi ya VAT. kwa kukuelimisha tu ni kuwa katika sheria ya kodi ta VAT kuna majedwali ambayo yanatoa ruhusu kwa baadhi ya bidhaa kutozwa kodi ya VAT. mfano ni unprocessed goods kama maembe. kwa hiyo kuna level ambayo VAT huanza kutozwa. mfano uliotoa wa maembe hauendani na kile ambacho watanzania wanalamikia hii serikali ya rais wetu mwema.

Gavana alieleza uhalisi wa sheria yenyewe ya VAT na jinsi inavyofanya kazi.
 
Naombeni ufafanuzi kwanini juzi serikali wamepiga marufuku taasisi za kifedha kuongeza gharama za miamala ingawa kwamba wameiongezea VAT ya 18%.......na bado mlichosema kuwa mtu wa mwisho ndiye analipia VAT..........

Marekani yenyewe na uchumi kuwa vizuri vile huu mfumo wa VAT hawautumii.......wanatumia sales tax..........


Kama haujaelewa nilichomaanisha katika huu uzi basi narudia tena kwa faida yako.....

Huo mfano na maelezo niliyotoa hapo juu si kitu kinachotokea Tanzania.....ila ni format ambayo ingekuwa nzuri kwaajili ya kupata kodi katika kila malipo yanayofanyika aidha yawe ya huduma au bidhaa.......

I hope vilaza wa BRN mtanielewa hapo ......maana m'meklemisha notes za sekondari na chuo ila kuzichambua ili muangalie ni nini kinafaa na hali yetu ya uchumi vichwa vimekuwa ni vigumu kama nazi za mkomazi.....
 
Mtoa mada, nenda kwanza kajiandikishe pale chuo cha kodi (usome diploma, degree au masters ya taxation), mimi nitalipa ada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…