Tujadili kuhusu "VAT"

Tayari raia wanaojua kutetea mifumo ya udhulumishi wamefika kutetea huu ubadhilifu.......kama ninachokisema si sahihi......ni kwanini mabenki yamekatazwa kuwatoza wateja ongezeko la VAT ili wao waikwepe........tumia akili nyepesi tu utapata majibu.......usipende kujiaminisha upo sahihi kwa kutumia ushahidi wa vitu vinavyoendelea kimakosa........

Mfano mdogo ni hata rushwa kuna watu wameklemisha kuwa unapifanya kosa la balabalani basi ni utaratibu kumpatia trafiki kitu kidogo wakati kiuhalisia hilo ni kosa lakufungwa kabisa ila kuna watu huwa wanaona hii ni halali na ni haki kufanya.
 
Mimi nakubaliana na ii kitu kua anaekuuzia ndio anaetakiwa kulipa io kodi
Mfano hai:Mim niliwai kwenda duka moja pale k koo kununua bidhaa mbali mbali ni kama taa flani za mapambo thamani ya zile bidhaa ilikua ni kama elfu 80 yule muuzaji wakati anataka kunipa risit akaniomba anikatie ya njiani MEANs anikatie risit kwa kuandika bei ya chini sana kuliko bei halisi ya bidhaa nilizochukua
 
Yaani mkuu umechanganya madawa ile mbaya!!utaratibu wa VAT hauko hivyo kabisa!!kwanza elewa kuwa kuna sifa maalum kwa mfanyabiashara kuwa mkusanya ji wa kodi ya ongezeko la thamani,si kila mfanyabiashara ana sifa hiyo,na yeye anakusanya hiyo kodi kwa niaba ya serikali kutoka kwa mtumiaji,na baada ya kupeleka returns zake kila mwezi wanaangalia mauzo ghafi na manunuzi yake,ndio wanajua kama unadaiwa au unadai,na sio kila bidhaa mfano maembe hayatozwi vat.ni somo kubwa sana,Ila wewe umechemka sana na hata kwenye kukokotoa VAt ni tofauti kabisa na unavyofanya eti kama vat ni 10% mfano wa 30000 ni elfu 3000???mkuu unachekesha hii ni fani ya watu sio unavyofikiria..Rudi darasni upate mwanga japo kidogo.
 
Yaaninhuyo jamaa hana analojua juu ya VAT kabisa,hata kukokotoa vat tu hajui anadhani ni suala tu la kuchukua mfano asilimia 10 ya 30,000 ni 3000!!!ndio vat ina kokotolewa hivyo??
 
umenierimisha sana mkuu .kumbe benki wanataka kutuibia kwa kuongeza bei ya kutumia atm kwa mteja wakati ni wajib na jukumu lao .
Jamaa amewalisha matango poli ile mbaya,hajui anachokielezea,mfumo wa VAT hauko hivyo kabisa,bei ya bidhaa au huduma unayonunua inakuwa na kodi ya ongezeko la thamani humo humo,yule muuzaji kama amesajiliwa na VAT yeye anakuwa ni mkusanyaji tu wa kodi hiyo kwa niaba ya serikali na kila mwisho wa mwezi anatakiwa kupeleka returns zake,,ambazo na yeye atatakiwa kuonyesha mauzo yake ghafi,ambayo ndio hayo aliyowauzia nyie na manunuzi yake aliyofanya,ndio wataangalia kama mauzo yake yanazidi manunuzi atapaswa kulipia hiyo tofauti,ila kama manunuzinyake ni makubwa kuliko mauzo ya mwezi husika atarejeshewa pesa iliyozidi,japo sio cash kabisa itabaki huko ila kama return yake ya mwezi unaofuata atadaiwa itapunguzwa kwenye hiyo credit balance yake,kwanza aelewe kuwa kila mfanyabiashara lazima awe na TIN(tax identification number)ila si kila mfanyabiashara lazima awe registered na VAT.
 

Kwakudanganya kwa makusudi au kwakutojuwa jinsi ya VAT inavyofanyakazi nineamua kukupa LIKE.

Yaani katika mfano wako wa maembe unadanganya kwamba VAT ni punguzo la kiasi anachopokea muuzaji kwa asilimia zilizopangwa na serikali. Kwamba kama embe ziliuzwa sh 30,000 mnunuzi hatalipa zaidi ya sh 30,000 bali muuzaji atabakiwa na kiasi pungufu ya sh 30,000. Nikufungue macho; kodi katika bidhaa inaongeza bei ya bidhaa hiyo na ongezeko hilo ndilo linalokwenda serikalini. Hivyo basi, Baresa atauza juice yake kwa sh 30,000 (hiki nikiasi kinachompa yeye faida au aka break even na kamwe hatapunguza 10% iende serikalini), juu ya hapo ndipo atamwongezea mnunuzi kwa 10% na hivyo kumfanya mnunuzi alipe sh30,000 plus ongezeko la 10% ambapo jumla itakuwa sh 33,000. Hapo sasa Baressa atapeleka sh 3,000 serikalini.

Mkuu rudi darasani tena, na kama huna uhakika wa unachokisema tafadhali usichangie mada za kisomi maana kwa kufanya hivyo unapotosha wanafunzi wanaosoma hapa na kujifunza.
 
Mkuu... huyu jamaa nadhani ana lengo la kuwafanya watu wawe wajinga zaidi... sijui ana lengo gani. .. au labda naye hajui maana ya VAT...
 
Walioko TRA au wachumi

Please explain VAT on Tourism

And Tourists are consumers and pays VAT

Sasa marejesho yanakuwaje kwa Tourists? TRA na Wizara ya Fedha mmejipanga?

Why Do Government charges VAT on its own money/revenue? - (Park entry fees) What is aim?
 
Maelezo ni mazuri sana na huenda yakashabihiana na mipango mizuri pamoja na taarifa zilizomo kwenye makabati ya wizara na taasisi zetu. Lakini alichoambatanisha mpiga domo kinaendana tofauti na uhalisia huu.
Ngoja nifuatilie katika nchi zingine kujua utofauti na ukweli lakini Tanzania kila kitu huenda kinyume nyume na dio maana RPC 'anavunja tamko la polisi' la kuzuia mikutano na mikusanyiko ya kisiasa!
 
Mtu aliyepata maendeleo kuliko wewe ni vizuri kuiga mfano wake.....

Japan imefanya mapinduzi ya Viwanda na kutengeneza magari miaka ya 70s/80s......Japan waliiga UK, Italy, France, German....
Hata USA waliiga Europe na Israel kutengeneza Cardilac na Hummer

So Japan ni koloni la Europe?????

Kenya wametuzidi kiuchumi na viwanda.... Bidhaa za Kenya ni bora sana....Tujilinganishe

South Africa, Botswana, Mauritious, Namibia.....

Is Tanzania only wildlife safari destination?

Au Mlima Kilimanjaro?

Who know Table Mountain

Drakensberg?
 
Pengine asilimia 18 kwa bidhaa na huduma ni kubwa mno kwa ujumla wake kutokana na utafaouti wa bidhaa na huduma, na umuhimu wake kwa jamii.

TRA wangeweka unafuu wa asilimia kwa mahitaji muhimu kama vile madawa na huduma za hospitalini, na kwenye usafiri wa mabasi, hali kadhalika katika vyakula.
 
kwa wale wenye kujitoa fahamu (sisi.....) na viongozi wake sijui kama watakuelewa labdaamuunge mkono mtoa mada
 
swali...mbona ukienda nunua UMEME au MAJI. tunalipa na VAT wakati kwa elim yako hiyo aliepaswa kulipa vat ni tanesco au idara ya maji...lakin nakuta kwenye risiti nalipia na VAT?
 
Sasa hapa ndio watanzania mjue kuwa wanaotufilisi hii nchi ni wasomi na masomo yao kuklemisha na si mataifa ya nje.............mimi hapo nimeonyesha mfumo ambao VAT inatakiwa kuwa na serikali iweze kupata mapato yake inavyotakiwa......na nikaandika kabisa kuwa huo ni mfano........na hata hivyo namna serikali wanavyokokotoa VAT si kama hapo juu maana hata ningekuwa sijui chochote ningeenda online halafu ningekuja kupaste tu vitu nilivyosoma...........lakini nilichofanya hapo ni kutoa namna ambayo ingekuwa nzuri ya kukusanya kodi ya serikali........

Ila tatizo ni kuwa wasomi wengi tanzania wapo vizuri kwenye kumeza vitu kama vilivyo bila kuvitoa dosari...........iwe ni mambo ya benki upande wa riba na makato au inshu za kodi kama hivi........hili taifa linahitaji wasomi ambao wanahoji mifumo na sio watu wanaokwenda shule wanajua tu kumeza hesabu halafu wanakuja kutumia walichojifunza kurudusha taifa nyuma kwa kuwanyonya wananchi kupitia mifumo ambayo sio rafiki kwa maendeleo ya wananchi achilia mbali ya taifa.............

So kwa wale ambao mnasema nilichosema sio kitu cha kueleweka wekeni mfumo halisi wa VAT halafu mtaona kama kuna mjumbe atawaelewa au ataona tija ya huo mfumo halisi.........



Ifike wakati wasomi tuwe watu wa kuhoji mifumo ambayo haitusaidii kuleta maendeleo.......leo hii raia wa kawaida kwanza hata haelewi nini maana ya kodi maana hajui inamaana gani zaidi anahofia itamzulumu........


WITH MY SOCIETY I STAND.
 
mtoa mada maneno mengi na mifano mingi yako ipo kimtizamo ila uhalisia vat analipa mtumiaji wa mwisho na ndyo maana kwenye hyo vat mzigo wote anabeba mtumiaji wa mwisho.japo ipo kwa kila hatua ila mfanyabiashara anaisaidia serikali kukusanya toka kwa mlaji wa mwisho na yeye ndye most affected.hvyo hizi taasisi za fedha zinaisaidia tu serikali kupata kodi yake kutoka kwa maskini mtumiaji wa mwisho.hyo ya mtoa mada ni mfumo wake ambao naona anaishauri serikali.bt kwa tz na jinsi vat ilivyo mzigo upo huku kwetu na c kwa mfanyabiashara wa taasisi za fedha.mtoa mada yupo kinadharia zaidi.
 
T
Tofauti yako na mtoa mada ni ipi hapo. Kabla haujakosoa soma ukaelewa. Muuzaji si lazima amwambie mnunuaji kwamba laki mbili na vat, maana ya mtoa mada ni kwamba wewe piga faida zako then ongeza vat kisha ndio muuzie mnunuzi.
 
Hii ndio maana ya vat sijui huyo jamaa kaitoa wapi maana yake. Vat ni value added tax kwa maana kuwa ni kodi juu ya thamani ya kitu au huduma.
Huyu Killaza wetu kaja kudanganya watu humu! sasa mamuma wengine wako wanasema et wameelewa somo! hawaendi hata kwenye supermarket zetu waone kwenye receipt wajue ni nani kalipa VAT kati ya muuzaji na mnunuaji!!!!!
Anayenunua ndo anayelipa VAT!!!! Toa mifano yako lukuki lkn ukweli ni huo, na kama sivyo hatuna serikal maana raia watakuwa walishaibiwa tangu Vat imeanzishwa!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…