Tujadili hoja hizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili hoja hizi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mundali, Oct 11, 2010.

 1. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tanzania tupo kwenye kipindi muhimu sana cha uchaguzi. Katika wakati huu tujadili namna ya kuwatambua viongozi bora. Baba bora ni yule anayejituma kila wakati kuhakikisha maisha bora kwenye familia yake. Hali kadhalika kiongozi bora ni yule anayejitolea kwa ajili ya jamii yake. Na daima nyumba bora hujengwa na wenye nyumba. Tuwaangalie hawa kwa darubini kali.
  1. Tuliwapa shirika likiwa na treni, mabasi ya abiria na magari ya mizigo pamoja na meli, waliviendelezaje?
  2. Shrika la ndege likiwa na ndege takribani 9 (Twin orters, Forker Friendships, Boeings n.k) wamelifikisha wapi?
  3. Viwanda vya nguo (Urafiki, Sunguratex, Kilitex, Mwatex, Mutex, Mbeyatex n.k), viko wapi?
  4. Viwanda vya ngozi, kusindika nyama, maturubai, radio, viatu, mlolongo ni mrefu. Vinaendeleaje?
  5. Sekta ya kilimo na vyama vya ushirika na mabenki yaliyojihusisha na kilimo nayo vipi?
  6. Uvuvi, TACOSHILI, uwakala wa meli na mengineyo je?
  Mambo ni mengi ila tutasema ubinafsishaji, simple answer.
  Turudi ndani ya nyumba yetu.
  1. Iko wapi SUKITA?
  2. Iko wapi SUWATA?
  3. Uko wapi mradi wa mabasi ya wanafunzi (Umoja wa vijana)?
  Kama nyumba yetu tumeshindwa kusimamia rasilimali zake, tutaweza kusimamia za jamii yetu?
   
Loading...