TUJADILI HILI.

TUJADILI HILI.

mustry75

Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
84
Reaction score
89
Habari Wakuu wa Jukwaa Hili.

Tumshukuru Mungu kwakuwa bado tuna uhai mpaka muda huu.

Kuna hili swala linalosemwa sana kupungua kwa Ukwasi mtaani, huwa maranyingi swala hili likiongelewa watu wengi hubadili mada kutoka Hoja ya maswala muhim ya uchumi wa nchi kuwa swala la kisiasa, kwakiasi kikubwa nashindwa kuona ninamna gani nzuri kuwasilisha yale ninayo yaona mimi huku mtaani kuhusu hili swala ila ngoja niseme hivi.

Niliwahi kukutana na hili swali mwaka 2016 mwanafunzi mmoja chuo kimoja hapa nchini alipo pewa Assignment akaulizwa Discuss CAUSES OF CURRENT LIQUIDITY CRUNCH IN TANZANIA.

Alijitahid sana kuandaa points zake ila alipo wasilisha aliambiwa kajibu siasa aliumiza kichwa sana ila kimsingi yale kwa maoni yangu ndio yalikuwa majibu sahihi kwawakati huo.

sasa Embu ona hili hali nimbaya kweli mtaana pesa imeadimika hii ni sifa ya pesa yoyopte duniani ila kuna vyombo maalum ambavyo vina regulate hii hali. Naweza kusema hapa nchini hichi chombo kina yumba au kinaenda kisiasa zaidi kwani ukisema haya utaambiwa Tulikuwa tukitegemea pesa za mafisadi, Ijalie nikweli tumeambiwa wamezitema na tunaendelea kuzitema kwelikweli hata zile za halali hili ndio linalo pelekea pesa kuwa ngumu na hii hali inahitaji tuseme kuwa imetosh sasa serikali ina wajibu wa kuingiza pesa kwenye mzunguko pesa imepungua kwa kiasi kikubwa sana na hii inatokana na nini??

Hapa kuna njia kadhaa ambazo hutumika kupunguza pesa kwenye mzunguko kwenye huu uzi siwezi kuzieleza zote ila naweza kuelezea moja tuu

Miongoni mwa njia hizo ni kama ile
1. Reducing Government Expenditure
2. Tax
3. Required reserve
Nanyinginezo nyingi kwakupitia njia hizi serikali inaweza kupunguza pesa kwenye mzunguko.

Kweli.!! tunahitaji kusema pesa imepungua mtaani kwani embu tuangalie tuu hii kodi...

kodi nijambo zuri kwa serikali kwani ni chanzo cha mapato kwahapa kwetu tunaweza kusema ndio chanzo kikuu cha mapato ya serikali, lakini hii kodi ya sasa imesababisha pesa kupungua kwa kasi mtaani tena istoshe ikumbukwe wakati huohuo matumizi ya serikali yamepungua sana{ rejea sera ya kubana matumizi} hivyo serikali imezichukua pesa zake kwakiasi kikubwa sana huku mtaani. Angalia mfano huu wa kodi leo TANESCO ukinunua umeme wa 1000 utaambiwa cost ni 819.68 VAT 18% = 147.53 EWURA 1%= 8.20 hii inamaana nimelipa kodia kwa buku yangu hio shilingi 147.53 wakati huo huo nimekatwa shiling 11 kama transaction cost TIGO PESA na nakatwa shiling 2 VAT tena yaani kwenye transaction 1 ninalipa VAT mara mbili. bilashaka tunapaswa kujua serikali inachukua pesa yake ambayo iko kwenye mzunguko kwa kasi na spending imepungua ukilinganisha na kipind chanyuma kabla ya vyeti feki wafanyakazi hewa na wale wote waliokuwa wakiibia serikali. Hii ndio inasababisha mtaani kumekuwa kugumu

Tuseme jamani kuwa pesa haipo mtaani sbabu serikali inaichukua kwa kasi na ina irudisha kidogo sana.

NAOMBA KUWASILISHA.
 
Sounds like you’re talking inflation. Was it there to begin with?

One popular method of controlling inflation, is through a contractionary monetary policy. The goal is to reduce the money supply within an economy by decreasing bond prices and increasing interest rates.
 
Back
Top Bottom