Tujadili dhana ya uchochezi

Sharif

JF-Expert Member
Mar 13, 2011
2,450
1,777
Ni wakati mwafaka kujadili haka kadhana ka "uchochezi"

Awali uchochezi ulikuwepo katika sheria za Uingereza na Wales kabla ya kufutiliwa mbali mwaka 2008.
Katika sheria hii ya mzungu, uchochezi "incitement" ulitafsiriwa kama..
"shawishi, hamasisha, lazimisha, tisha, chochea au sababisha mtu atende uhalifu.

Dhamira ya uchochezi "mens rea" hulenga katika kumshawishi mtu ili atende jinai .

Wajuzi karibuni kwenye weledi wenu mtuhabarishe.
 
Kwa Tanzania uchochezi ni kumpinga au kumkosoa Magufuli.

Pia kuota mabaya juu yake nao ni uchochezi.

Kuhoji uhalali wa pihechidii yake kunaweza kukupoteza.

Kuchapisha data za utafiti ni uchochezi iwapo zitapingana na hisia zake hata kama data ni za kweli.

Media itakayo report habari zisizomfurahisha zitatuhumiwa kwa uchochezi.
 
Kwa Tanzania uchochezi ni kutoa mawazo ya kupinga viongozi na mambo yao
 
Nilishawaambia kinachochochewa ni moto tu hizi nyengine ni mbwembwe..
 
Back
Top Bottom