Tuition na kutimua wanafunzi ni ruksa?

Brightman Jr

JF-Expert Member
Mar 22, 2009
1,225
232
Wakuu wa jukwaa kulingana na title hapo juu; naomba kufahamu mambo mawili kwa kuwa sasa yanafanyika bila kizuizi chochote.
1. Shule ya msingi hapa kijijini siku hizi madarasa yamekuwa ni vyumba vya kufundishia tuition nyakati za jioni, na hao wanaofundisha ni walimu wa shule hiyo. Je, sheria inasemaje hapa?
2. Katika shule hiyo mwalimu mmoja wa masomo ya Kiingereza na Haiba amewatimua wanafunzi saba katika darasa analofundisha wakati wa mtihani wa masomo hayo; kisa watoto hao aliwataka wampatie pesa ya kwenda kuburuza mitihani na kutokana na uwezo duni wa wazazi wanafunzi wakatimuliwa ndani ya chumba cha mtihani. Sheria inasemaje kuhusu suala hili?
Natanguliza shukrani
 
mii siyo mwanasheria lakin naomba nichangie kidogo
1) kuhusu madarasa kutumika kufundisha tuition je ni remedial classes kwa wanafunzi wa shule hiyo?au ni hata wa mtaani? ama ni rremedial classes kwa anafunz husika siyo kosa kisheria. ila kama ni kwaajli ya wanafunzi wa mtaani tu ni kosa kisheria na wasiliana na afisa elimu msingi akusaidie juu ya hili.

2)wanafunzi kutimuliwa, hapa pana utata sana, kwani mitihani hii ni ya terminal au ni majaribio ya darasani(tests) manake ukiangalia ka makini mitihani ya majribio kwa shule karibu zote z msingi huwa wanalipia na hii ni kutokana na hali halis mashulen hakuna mafungu na wanafunz hawalipi ada. kwa maana hiyo unakuta shule ya msingi mwaka mzima inajiendesha bila hata ya senti tano tka serikalin na waalim wanakosa vitendea kazi. kumbuka mwisho wa siku mwl anategemewa afaulishe wanafunzi na njia mojawapo ya kuwafanya wafaulu ni pamoja na kuwapa majaribio mengi.

inapotokea mwanafunzi hajachanga majaribio mawili matatu na pengine ulimbeba kwa kufanya juu ya migongo ya watu basi safari nyingine ana haki ya kumtoa nje kwani huyu ni kupe kabisa. siku ya kwanza hana sawa utavumilia na ya pili tena na ya tatu jamani tunajua ugumu wa maisha ya kijijini basi mzazi au mlez aje aseme na ajicommit kuwa atatoa kuliko kutegemea vya bure tu ambavyo hao wenzie pia wanaumia pa kuvitoa.
 
Nashukuru mkuu kwa kunipa mwanga juu ya mambo niliyouliza. Kimsingi madarasa hayo hayatumiki kama remedial classes bali ni biashara ya baadhi ya walimu ambao wameteua baadhi ya wanafunzi toka familia ambazo ziko well off na kuwapa mafunzo ya ziada na kulipwa ujira wao kila mwezi.
Kuhusu mitihani ni kwamba hii ni mitihani ya nusu muhula ambayo matokeo yake huingizwa katika kadi za maendeleo ya mwanafunzi na mzazi hupewa taarifa ya maendeleo kitaaluma ya mtoto wake.
 
Back
Top Bottom