Tunakushukuru mtoa mada hii kwa kuileta hapa jamvini ili wanataaluma wenzako (walimu) waweze kutoa michango yao mbalimbali kwamba tatizo la tuition ninini? ikizingatiwa kwamba hapo kabla haya mambo hayakuwepo na bado kiwango cha uzamivu naamini kilikuwa kizuri kuliko ilivyo sasa.
Kwa haraka haraka nadhani tuition ni matokeo ya wanafunzi kutopata muda wa kutosha ili kuhudhuria masomo, walimu kutotumia ipasavyo muda uliopangwa kwa lecture na badala yake kufanya mambo yao kutokana na kazi yenyewe (taaluma ya ualimu) kutothaminiwa na mwajiri mkuu (serikali). Yote mawili au uwezo mdogo wa wanafunzi na walimu na hivyo kuchukua muda mrefu kufidia vitu ambavyo mwanafunzi alitakiwa awe anafahamu kabla ya kuwa katika level hiyo ki elimu.
Mwisho kabisa, ni bahati mbaya kwamba tuition imeshakuwa utamaduni.utashangaa kwamba mzazi ana mpeleka mwanafunzi tuition kwa ajili ya pre std one. Kama taifa tuone jinsi hali ilivyo mbaya ki elimu.
[Asante kwa udadafuzi huu]
Kwani tutition inaweza kuwa tofauti na discussion? Maana kuna discussion watu wengine huwa mabubu wanaandika kinachosemwa tu hata kama ni KASA.wafanyeje wakati wananyimwa mikopo...............acha wafundishe tuition pengine itawasaidia kwani wengine wanategemewa kwao................
Kwanza kabisa napenda kujahamisha wanajf kuwa mimi ni mwalimu mwenye shahada ya uzamili jamii katika elimu, shahada ya elimu katika elimu ya watu wazima zote hizi kutoka chuo kikuu cha Dar es es Salaam, pia nina stashada ya elimu kutoka chuo cha ualimu korogwe ninauzoefu wa kufundisha miaka sekondari maika 7. Napenda kusema kuwa jina la Mabuba ni jina langu halisi na sio jina kivuli.
Naweza kutofautisha kati ya Tutorial na tuition. Hapa ninachozungumzia ni TUITION. Labda wanajf tujadili ukweli (issue) kuliko mtu. Tution ile inafundishwa na wanafunzi waliomaliza udsm, somo ni uchumi, kila mtu hulipa shilingi za kitanzania 500/= kwa kipindi. Mimi nadhani wote wanaotetea ni waathirika wa tuition.
Jamani tuition za aina hii hazijengi taifa. Hebu fuatilia wanafunzi wengi waliosoma tuition, utakuta hajuikujenga hoja, ni mtu wa kuelewa maswali kuliko dhana ya jambo. Wanakariri kuliko kuelewa. Pia wajf kuna vitabu TUITION yaani vile vya maswali na majibu, vitabu hivi kwa sasa ndio vianaongoza kwa mauzo ya vitabu.
Tujadiliane ukweli kuliko kuukimbia, tutatue tatizo
Kwa haraka haraka nadhani tuition ni matokeo ya wanafunzi kutopata muda wa kutosha ili kuhudhuria masomo, walimu kutotumia ipasavyo muda uliopangwa kwa lecture na badala yake kufanya mambo yao kutokana na kazi yenyewe (taaluma ya ualimu) kutothaminiwa na mwajiri mkuu (serikali). Yote mawili au uwezo mdogo wa wanafunzi na walimu na hivyo kuchukua muda mrefu kufidia vitu ambavyo mwanafunzi alitakiwa awe anafahamu kabla ya kuwa katika level hiyo ki elimu.
Mwisho kabisa, ni bahati mbaya kwamba tuition imeshakuwa utamaduni.utashangaa kwamba mzazi ana mpeleka mwanafunzi tuition kwa ajili ya pre std one. Kama taifa tuone jinsi hali ilivyo mbaya ki elimu.
[Asante kwa udadafuzi huu]
SUA hakuna huo ujinga wa tuition tuition hadi university!! MUNGU atusaidie yalianza madesa tukasahau vitabu kwa visingizio vya ukata sasa jipu lizidi kuvimba waungwana wahitimu wa UDSM kemeeni hili madogo ndo wana chepuka njia hivyo kaaaazi kwelikweli
SUA ndo pale mnaposoma mambo ya uchumi wa nyumbani na lishe then mnaenda kuwa Ma bank teller??!!! nyie hamuhitaji tuisheni vitu vyenu laini vinaeleweka hata ukiwa umelelala pale Hostel 5 karibu na round top unaelewa tuu...hahaaaa
Afadhali na wewe umeliona hilo. Kuna watu hujadili vitu visivyo na tija kabisa. Pitia mjadala wa Chuo cha Morogoro. Binafsi naona hizi hasa ndio sababu za nchi yetu kuwa hivi. Maana unaweza ukasoma hoja ukakumbana na matusi au kebehi. Watu hawajadili facts. Inasikitisha na pia inawezekana ndio mfumo wa elimu uliotufikisha hapa.Kigogo,
Naomba uhamishie hii post yako kwenye jokes. Watu wana familia, zinazokula na kuishi kwa sababu ya hiyo shule na kazi unazojaribu kuzidhalilisha. Tafadhali sana watendee haki wenzio kama ambavyo ungependa kutendewa. Tukianza kuzichambua shule na ajira za watu sina hakika kama wewe mwenyewe utapona!!
Jamani ninachokiongelea hapa ni jambo la ukweli na sio uzushi. Pia lazima tutofautishe programme na tution. Pre entry ni programme na sio tution. WanaJF tafadhari kama yupo yoyote anayeishi Changanyikeni akaulize hilo. Hii ni aibu kuu kwa UDSM.
Jana jioni nilikuwa natokea maeneo ya Changanyikeni. Changanyikeni ni eneo lililokaribu kabisa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Nilikutana na kundi kubwa la wanafunzi wakitembea kwa mguu na wengine daladala pia bajaji. Nilizani wanaandamaa juu ya mikopo, haikuwa hivyo.
Niliamua kuwauliza nini hasa kimetokea, walikataa kuniambia nini hasa kimejili. Niliendelea kudodosa, ndipo nilipopata jibu wanatoka tution (mimi huita TUISHIENI) niliumia sana moyoni, mimi ni mwalimu ninajua madhara ya tution kwa taifa letu. Tokea kuanza kwa tution kuanzia elimu ya msingi na sekondari na sasa elimu ya juu, tumekuwa na wanafunzi wasioweza kufikiri, wasiosoma vitabu, wasiojenga hoja bali kukurupuka, wasiojitambua, wategemezi kinadharia na vitendo, watazamishwaji wa mitazamo na mambo mengine kama hayo.
Naumia sana, nilianza kuona Open University na sasa UDSM, yawezekana kabisa hili lipo kwa vyuo vya elimu ya juu vyote. Wanajamii naomba sana tupige kelele kukomesha hili. Wakati tunapiga kelele tuangalie yafuatayo:
1. Je tution chanzo chake ni nini?
(a). uhaba wa walimu
(b) Ugumu wa maisha ya walimu
(c) Ukosefu wa ajira kwa Vijana
2. Sera ya elimu ina matatizo
3.Elimu yetu ni utazamishwaji wa mawazo ya wakoloni/ mabwanyenye/ mabepari?
4. Walimu wetu ni wabobevu wa taaluma zao?
5. Msingi wa kuandaa walimu wetu ni bora
6. Je wanafunzi wetu ni wavivu
7. Turuhusu tution kwa walimu bora na sio bora walimu
8. kwa chuo Kikuu cha Dar es salaam
(a). mnalifahamu hilo
(b). tatizo ni nini?
(c). je hao ndio aina ya wanafunzi mnaowadahili?
(d). Mnawahadhili bobevu wa fani mbalimbali nini mchango wao katika hili
Wanajamii elimu ndio msingi wa taifa endelevu tusitegemee wanafunzi wa TUISHIENI waje wajenge taifa letu. Naumia sana.
Tujadiliane
Je wewe ni mojawapo wa wanafunzi? If yes then the discussion ends.Many thanks Injinia......! Watu hupenda sana kudandia gari kwa mbele na kuanza kudiscuss issues kabla ya kujua ukweli halisi ni upi!
Tutorial /Tuition Univeversity ndio mahala pake.....sasa na nashangaa watu mnashangaa hapa tu kisa mmekariri kuwa TUITION hutumika kumaanisha masomo ya ziada baada ya kutoka darasani in case mwanafunzi hajaelewa au hakucover topics fulani kwa malipo ya ziada! Hii ni applicable kwa shule za msingi, Chekechea & Secondary (O & Alevel)!
Tuition /tutorial anayosema hapa mwanafunzi halipii extra money, akisha lipa ada inatosha......! Please don't confuse things! Kuanzia mtoa mamda mpaka wa changiaji wamechanganya mambo hapa!
Sorry Mkuu Mabuba unaweza kutuambia unaelimu ya level gani na umesoma vyuo gani?(option). Naoana uelewa wako ni mdogo sana kuhusu mfumo wa vyuo vikuu!
Nadhani hukuwaelewa, labda walikuambia wanatoka kufanya TUTORIAL na sio tution,Jana jioni nilikuwa natokea maeneo ya Changanyikeni. Changanyikeni ni eneo lililokaribu kabisa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Nilikutana na kundi kubwa la wanafunzi wakitembea kwa mguu na wengine daladala pia bajaji. Nilizani wanaandamaa juu ya mikopo, haikuwa hivyo.
Niliamua kuwauliza nini hasa kimetokea, walikataa kuniambia nini hasa kimejili. Niliendelea kudodosa, ndipo nilipopata jibu wanatoka tution (mimi huita TUISHIENI) niliumia sana moyoni, mimi ni mwalimu ninajua madhara ya tution kwa taifa letu. Tokea kuanza kwa tution kuanzia elimu ya msingi na sekondari na sasa elimu ya juu, tumekuwa na wanafunzi wasioweza kufikiri, wasiosoma vitabu, wasiojenga hoja bali kukurupuka, wasiojitambua, wategemezi kinadharia na vitendo, watazamishwaji wa mitazamo na mambo mengine kama hayo.
Naumia sana, nilianza kuona Open University na sasa UDSM, yawezekana kabisa hili lipo kwa vyuo vya elimu ya juu vyote. Wanajamii naomba sana tupige kelele kukomesha hili. Wakati tunapiga kelele tuangalie yafuatayo:
1. Je tution chanzo chake ni nini?
(a). uhaba wa walimu
(b) Ugumu wa maisha ya walimu
(c) Ukosefu wa ajira kwa Vijana
2. Sera ya elimu ina matatizo
3.Elimu yetu ni utazamishwaji wa mawazo ya wakoloni/ mabwanyenye/ mabepari?
4. Walimu wetu ni wabobevu wa taaluma zao?
5. Msingi wa kuandaa walimu wetu ni bora
6. Je wanafunzi wetu ni wavivu
7. Turuhusu tution kwa walimu bora na sio bora walimu
8. kwa chuo Kikuu cha Dar es salaam
(a). mnalifahamu hilo
(b). tatizo ni nini?
(c). je hao ndio aina ya wanafunzi mnaowadahili?
(d). Mnawahadhili bobevu wa fani mbalimbali nini mchango wao katika hili
Wanajamii elimu ndio msingi wa taifa endelevu tusitegemee wanafunzi wa TUISHIENI waje wajenge taifa letu. Naumia sana.
Tujadiliane
Mkubwa siku hizi hakuna Chuo kikuu kishiriki... ni fully fledged university na inaitwa MUHAS kwa kifupi.Jamani pamoja na kukubaliana na hali hii inawezekana kabisa ikawepo hapo UDSM, naomba niseme kitu ambacho nina uhakika nacho kwa vile kuna watu ninawafahamu ambao wanafanya kazi na wanasaidia katika hili kwa malipo kabisa.
Chuo kikuu kishiriki cha madaktari Muhimbili hili suala lilianza siku nyingi huenda ni miaka 3 au 4 sasa. Mwenye nafasi afanye uchunguzi. Pale Aga khan kuna Dr Shaffik ana madarasa ya tution kabisa ambayo wateja wake wengi ni mabinti wa MD pale Muhimbili na imekuwa muda mrefu tu!
Natumaini kwa MD yeyote aliyepo hapa JF atakubaliana na mie kuhusu viwango vya madaktari wanaotoka Muhimbili sasa vikoje. Sijui tunajenga taifa la namna gani lakini kwa ujumla nchi yetu inahitaji overhaul ya nguvu ndani ya system mfumo wetu ni mchafu umekuwa na CCM haitaweza kwa vile haina dhamira tena inafaidika nayo.. Nawakilisha
Pass mark ya Udsm ni 40%,wewe unataka kusema nini au unataka kuharalishaTuition chuo kikuu kwa hiyo 40%?Weye washangaa tuition? Waijua pass mark ya mitihani udsm? Ulizia!