Tuition centre zafungiwa mjini Kahama

Tuition centre zafungiwa mjini Kahama

MBUTEGWANE

Member
Joined
Jan 13, 2015
Posts
33
Reaction score
8
Vituo vyote vinavyotoa huduma ya masomo ya ziada kwa watoto alimaarufu "tuition centre", vimefungiwa na mamlaka husika.

Msako mkali ulifanyika huku kukiwa na polisi.

Vijana waliohitimu kidato cha nne na sita ambao hawana ajira ya kudumu na kuamua kubuni njia mbadala ya kujipatia kipato, ndio walioathirika na sakata hili.
 
hivi tution bado zinaendela hadi siku hizi, zamani wakati mdogo nilikuwa nasoma tution nilipokua nikagundua nilikuwa napoteza hela za wazazi tu
 
mkuu hujatuambia kwanini wamezifunga ?? watu si wanalipa pesa zao binafsi tatizo liko wapi? na kama huduma ni mbaya wasingepata wateja kwahiyo zingejifunga zenyewe au vipi ? hiki ni chanzo kizuri cha ajira sielewi kwanini wazifunge wakati waalimu hawatoshi mashuleni labda utufafanulie mkuu
 
hivi tution bado zinaendela hadi siku hizi, zamani wakati mdogo nilikuwa nasoma tution nilipokua nikagundua nilikuwa napoteza hela za wazazi tu

Tuition center zipo nchi nyingi, hata za kitajiri. Nimeziona Korea, Japan na Indonesia binafsi. Nyingi sio center moja kama zetu, zinaendeshwa kama mashirika na utazikuta katika kila mji. Zingine hata hufungua branch nje ya nchi kama KUMON ya Japan.

Siku ya kawaida ya mwanafunzi wa Kijapani:

Saa 2-9- shuleni
Saa 9-9.30 usafi ( walimu na watoto wanasafisha shule zao )
Saa 10- 12 michezo katika klabu zao za shule.
Saa 12-1 mlo wa jioni nyumbani
Saa 1-3 usiku - tuition

Jumamosi- jumapili
Saa 3-7 michezo shuleni katika klabu zao kama basketball, soccer etc

Saa 12-3 usiku Tuition
 
Vituo vyote vinavyotoa huduma ya masomo ya ziada kwa watoto alimaarufu "tuition centre", vimefungiwa na mamlaka husika.

Msako mkali ulifanyika huku kukiwa na polisi.

Vijana waliohitimu kidato cha nne na sita ambao hawana ajira ya kudumu na kuamua kubuni njia mbadala ya kujipatia kipato, ndio walioathirika na sakata hili.

Mbona umekurupuka? Sababu nini?
 
Mtoa mada pengine bado ana usingizi...tuvuteni subira akiamka atatufafanulia vizuri....
 
Binafsi shule nilosoma advance walimu walikuwa hawafundishi, isingekuwa tuition na PCB yangu ningeishia kupata div 5.

Thanks to Mr. Mlewa, Vice wakali wangu wa phs na chem, maisha saaaaaafi
 
Back
Top Bottom