Socratic
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 568
- 308
Kauli ya askofu Pengo kwa maoni yangu inaweza kuangaliwa kwa falsafa tofauti kama ifuatavyo.
1.Kiimani-Alichosema kuhusu free will ( uhuru wa kuamua) ni sahihi na hakuna mkristo wa kweli awezaye kupinga hili kimaandiko (irrefutable) katika ulimwengu wa kiroho, wanaopinga wanatumia nadharia nyingine.
2.Kisiasa-Alichosema askofu Pengo si sahihi kwa vile kina maslahi kwa makundi fulani kisiasa. wapo wanaodai katiba inayopendekezwa ilishachakachuliwa na kwa hiyo haifai na ndiyo maana wanaona maaskofu waliotoa waraka wako sahihi kuwashawishi waumini wao waipigie kura ya hapana.
3.Kijamii-Askofu Pengo yuko sahihi kwa alichokisema maana kikatiba kila mtu anayo haki na uhuru wa kutoa maoni yake bila kubughudhiwa na mtu yeyote. Na Askofu ametumia haki na uhuru wake wa kutoa maoni yake kama mtanzania yeyote. Kuwa askofu hakumpokonyi uhuru huo. Hapa JF watu wana mitazamo tofauti kuhusu mambo mengi lakini ndio msingi wa kuwepo jukwaa hili. Kila mtu anao uhuru kuchangia na kutoa mawazo yake.
4. Kisheria- Alichosema askofu Pengo si sahihi kwa vile kuna sheria ya collective responsibility kwenye canon law. Yeye kama mjumbe wa TEC hakufanya vema kupingana na tamko lililotolewa na maaskofu wenzake maana linaweza kuwachanganya waumini ambao husikiliza na kufuata maelekezo kutoka kwa viongozi wao na pia kuwaembarass maaskofu wenzake.
Kwa minajili hiyo askofu Pengo ametumia falsafa namba 1 na namba 3 katika kile alichosema na hivyo yuko sahihi na watu wengine wanampinga kwa kutumia falsafa namba 2 na 4 na hivyo hayuko sahihi.
Swali ni je? Askofu Pengo alikuwa na haki kutumia falsafa alizotumia kutoa kauli yake? kama ndiyo kwa nini? na kama sivyo alipaswa kutumia falsafa gani na kwa nini? Wapi ulipo mpaka kati ya falsafa moja na nyingine?
karibuni tuchangie.