karama kaila
Senior Member
- Jan 30, 2015
- 122
- 60
(25) Kazi na sifa za Kiongozi wa Chama
i) Atakuwa kiongozi mkuu wa Chama na Mwenyekiti wa kikao cha Mkutano Mkuu wa kidemokrasia
ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na maafisa wa ACT pamoja na vikao vya chama;
iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu baada ya kushauriana na kukubaliana na Mwenyekiti wa Chama Taifa na uteuzi kuthibitishwa na Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii;
iiii) Kuteua wasemaji wa kisekta ambao pia watakuwa ni wenyeviti wa Kamati za Makao Makuu;
v) Kuteua Naibu Kiongozi wa Chama kwa kushauriana na Kamati ya Uongozi atakapoona haja hiyo;
vi) Kiongozi wa Chama anaweza kuteua mwanachama mwingine mwenye mchango maalumu kuingia katika vikao vya chama kwa kushauriana na Mwenyekiti na Katibu Mkuu kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo kwa maslahi ya chama;
vii) Kupendekeza majina ya washauri wa chama baada ya kushauriana na Mwenyikiti;
viii) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa Chama katika mambo ya kitaifa na kimataifa;
ix) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa;
x) Ataendesha vikao vya Kamati za Kisekta ili kutengeneza misimamo ya kisera ya chama na kuwasilisha mapendekezo ya kisera katika vikao vya chama kwa maamuzi
xi) Iwapo Kiongozi wa Chama hayupo kwa sababu yoyote ile na pale ambapo hakuna Naibu Kiongozi wa Chama, basi Mwenyekiti wa Chama atamteua moja ya wasemaji wa kisekta kuwa Kaimu Kiongozi wa Chama;
xii) Iwapo kiti cha Kiongozi wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama, maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, Naibu Kiongozi wa Chama au kama na yeye hayupo basi aliyechaguliwa kutoka miongoni mwa wasemaji wa kisekta, atashikilia nafasi yake kwa sharti kwamba Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi kumi na miwili tangu kuwa wazi kwa kiti hicho kwa ajili ya kuchagua Kiongozi wa Chama, mwingine.
xiii) Mtu atakayechaguliwa kuwa Kiongozi wa Chama lazima awe na sifa za kuwa mbunge
xiiii) Endapo Kiongozi wa Chama atashindwa katika uchaguzi wowote wa kiserikali, Halmashauri Kuu ya Taifa itabidi ikutane katika kipindi kisichozidi miezi sita tangu kufanyika kwa uchaguzi huo ili kujadili mazingira ya kushindwa kwake na kupiga kura ya siri ya kuamua kama Kiongozi wa Chama anastahili kuendelea na nafasi yake au la. Kiongozi wa Chama ataendelea na nafasi yake endapo zaidi ya nusu ya wajumbe watapiga kura ya kuwa na imani naye.