Tuisapoti Taifa Stars iliyopo huko Afrika Kusini kwenye michuano ya COSAFA

10cd63acc36d815e9b8c05a35387ad75.jpg
 
starsKikosi cha Taifa Stars kesho kinatarajiwa kushuka dimbani kutupa karata yake katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kombe la COSAFA dhidi ya Zambia huku kikiwa na mshambuliaji mpya John Bocco.Hayo yamebainishwa na Afisa wa Habari Shirikisho la Soka nchini (TFF), Alfredy Lucas kwa kusema mechi ya kesho kuna uwezokano wa kumkosa mshambuliaji Mbaraka Yusuph ambaye ni majeruhi ambapo amedai licha ya Kocha Mkuu Salum Mayanga kumuita Bocco katika michuano hiyo lakini pia atatumika katika kuongeza nguvu kwenye kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.Kesho timu yetu ya taifa inashuka tena dimbani katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya COSAFA dhidi ya Zambia, mechi hiyo ni mchezo muhimu sana kwetu na nimewasiliana na Mwalimu na miongoni mwa vitu alivyovifanya ni kumjumuisha John Bocco katika kikosi. Kwa hiyo Bocco yupo Afrika Kusini na sababu ya kuwepo kule ni kuchukua nafasi ya Mbaraka Yusuph ambaye katika mashindano haya wakati wa mazoezi alipatwa na majeraha” alisema Lucas.Naye Meneja wa Taifa Stars Danny Msangi amesema “maandalizi ya kikosi chetu cha Taifa Stars yanaendelea vizuri. Vijana wetu jana walifanya mazoezi jioni pia mwalimu alikuwa anaangalia 'video' Zambia ambayo anayo na akawafundisha wachezaji nini cha kufanya, kwa hiyo tunashukuru Mungu wachezaji wote wapo vizuri kasoro Mbaraka ambaye ana maumivu na tunategemea mchezo huo wa kesho kuwa mzuri kwa kupata ushindi ili tuweze kuwapa faraja watanzania".
 
Back
Top Bottom