Django
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 354
- 147
wakuu,
hivi karibuni kamati kuu ya chadema imekutana siku ya july 6 na july 7 kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo hali ya siasa nchini.
Jambo la kushangaza ni maazimio yaliyo fanywa na kamati kuu kutokana muhafaka waliofikia kama kamati.
Kama kweli chadema ingekuwa na viongozi wenye hekima, busara, uzalendo, wapenda amani na utulivu, wasinge fikia muhafaka wa kuanzisha 'red brigade'.
Badala yake viongozi hao wangeishinikiza serikali kuimarisha ulinzi kwenye shughuli za chadema katika kufanya siasa.
Hoja ya kusema chadema wataunda na kuimarisha 'red brigade' ili ilinde mali na viongozi wa chama, ni dhaifu sana na haiwezi kutolewa na mtu mwenye akili timamu.
Kazi ya ulinzi hapa nchini sio kazi ya vikundi kama 'red brigade', bali ni kazi ya vyombo vya dola kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria mbalimbali za usalama.
Kamati kuu ya chadema imejidhalilisha, na inapaswa watanzania tuipuuze kamati kuu ya chadema bila kujali itikadi zetu.
pole sanaa