Tuikubalie DR Congo kujiunga na EAC?

Rwanda na Burundi wako ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini migogoro yao imetushinda Tanzania, Kenya na Uganda mpaka leo. Imetuletea gharama kubwa na upotezaji mwingi wa muda na rasilimali, unadhani Kongo ambayo ni nchi kubwa ndiyo tutaiweza ?
Rwanda na Burundi migogoro yao ilikuwa ya ndani ilihali Drc Mashariki migogoro yao ilichangiwa sana na nchi jirani (Rwanda na Uganda) hivyo itakuwa rahisi wao kupunguza mivutano huko Kivu.
 
Rwanda na Burundi migogoro yao ilikuwa ya ndani ilihali Drc Mashariki migogoro yao ilichangiwa sana na nchi jirani (Rwanda na Uganda) hivyo itakuwa rahisi wao kupunguza mivutano huko Kivu.
Una uhakika kabisa na hichi ulichosema ?
 
Una uhakika kabisa na hichi ulichosema ?
Migogoro ya ndani ipo (tokea wakati wa Uhuru mpaka baada ya mauaji ya Lumumba).

ila uhusika wa hizo nchi jirani huwezi kuupuuza.
 
Tutaunda jumuiya zikipandana tu na kuacha lengo la kuifanya Afrika ijitegemee, mfano ; KENYA imo COMESA, EAC na IGAD, utitiri wa jumuiya, ilikuwa Afrika iwe na blok Kama 4/5 hivi, zenye malengo ya kuweka mambo sawa ili kishajiisha maendeleo baina ya nchi za kiafrika ila huu utitiri ni uoza mtupu !!! Maoni yangu
 
Nakubaliana na wewe mkuu, kwenye nchi changa zenye Uchumi mdogo kama zetu kupandanisha uanachama wa Jumuiya mbalimbali (Overlapping Membership) ni janga ambalo linazuia nchi wanachama kutimiza vizuri malengo ya baadhi ya Jumuiya.
 
Wadau wamechangia hoja nzito kwenye mada hii. Nami nimeona pia nichangie.

Kwanza, DRC kujiunga na EAC siojambo ambalo nilitarijia hivi karibuni hivyo basi ni mshangao mzuri kusikia kuwa DRC wanataka kijiunga na Jumuiya. Ukitazama vizuri siasa za Afrika Mashariki na kati na historia ya ukanda huu utakubaliana kuwa ni milima miwili peke yake ambayo haiwezi kukutana au kuungana haswa tangu mabadiliko ya uogozi katika nchi za Jumuiya na DRC.

Pili, sitaki kurudia hoja zilizowasilishwa awali kwenye uzi huu ila nigependa kuongezea mkondo mwingine kulingana na mtazamo wangu utakao egemea zaidi idadai ya watu na uchunguzi wa ramani ya Afrika ya Mashariki na kati.

Ni kweli kuwa DR Congo yapo madini mengi na ya dhamani ya juu sana ulimwenguni inayofanya dunia mzima kuitamania kwa ulafi mwingi hadi kunao waliotaka kuwangamiza WaCongo kwa miaka mingi tangu enzi ukoloni mpaka leo. Lakini hii haifai kuwa kigezo kikuu kwa kuwakubalia DR Congo kuingia katika Jumuiya.

Wala kutokuwa na amani na usalama dhabiti kwenye DR Congo kuwa kigezo kiku cha kuwakatalia au kuwaweka pembeni wakati huu wanapotaka kujiunga na Jumuiya.

Ukichunguza ramani ya eneo la Africa Mashariki na Kati sana sana kwa mtazamo wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, ni rahisi kwa wadau kuona vile DRC ni muhimu sana kimkakati (very important strategically) kwa sababu hio ndio njia fupi na rahisi kwa zote kuunganisha Bahari ya Hindi na Bahari ya Atlantik. Kumbuka wengi wame changia kuwa kigezo kikuu kinapaswa kuwa uchumi kwa hivyo kukiwa na miundo msingi ya barabara, reli na mawasiliano unao unganisha nchi hizi za Jumuiya, DRC na Bahari hizi mbili kutaweza kurahisisha kufanya biashara kwa eneo hili. Hii ndio sababu kuu nilisema hapo juu kuwa DRC kutaka kujiunga ilikuwa mshangao mzuri sana kwani ukingalia USA ilivyoundwa nikuwa ililetwa pamoja na vita vikuu moja wapo ya hiyo ni vita vya kunyakua maeneo kuenda magharibi mwa bara la Marekani kaskazini ili USA iweze kuenea kutoka Bahari ya Atlantic hadi Bahari ya Pacific kupitia California. Hapa Africa tunaona kuwa DRC inajileta yenyewe kutokana na hamu yake bila kushuritishwa.

DRC kujiunga na Jumuiya italeta faida ya kiuchumi katika sekta mingi sio kwa rasilimali ya madini tu. Hiyo idadi ya watu milioni themanini na tano ina uwezo mkubwa kukiwa na amani na usalama kwa mfano katika sekta ya elimu, ukulima na ufugaji na hata soko la bidha. Wakati huu kunao waliona hofu kuwa itaporomosha uchumi(GDP per Capita) na kuwa hali ya usalama DRC sio ya kuridhisha na mwisho kuwa rasilimali zake za madini zitavamiwa na nchi zingine za Jumuiya. Kwanza Kuporomoka kwa GDP per Capita hakufai kuwa hoja kabisa kwa sababu uwezo wa kiuchumi wa DRC bado haujaanzishwa wacha kutimizwa. Pili katika usalama, DRC itakuwa better off ndani ya Jumiya kuliko inje ya jumuiya. Nchi ambazo zimechangia katika mizozo ya usalama na vita nchini DRC ni majirani wa DRC na moja wapo ya nchi za Jumuiya. Kumekuwa na mizozo kati ya nchi za Jumuiya lakini hakuna vita vilivyotokana na mizozo hiyo. Kwa mfano kumekuwa na mizozo ya kiusalama kati ya Rwanda na Burundi, Rwanda na Uganda na migogoro ya kidiplomasia na uchumi kati ya Kenya na Tanzania lakini hakuna ule mzozo ulioleta tishio kwa Jumuiya au vita ndani ya Jumuiya kwa miaka ishirini sasa. Migogoro ndani ya Jumuiya itaendelea kuwa lakini haifai kufwanywa kimasksudi au kwa kiwango cha kutishia Jumuiya. Kwa maono yangu ningependekeza kuwepo na ofisi ya ubalozi ya Jumuiya ambayo itasimamiwa na Balozi wa amani, Usalama na mahusiano mazuri (peace, security and good relations) ambaye atakuwa anafanya shuttle diplomacy na kubisha hodi katika nchi yeyote ya Jumuiya ili kutimiza malengo yake na kutoa mapendekezo na riporti ambayo itatumiwa kufanya majadiliano au maamuzi ya ufahamu mwema (informed decision). Kumbuka mkataba wa Jumuiya inasema kuwa kunapaswa kuwa na ujirani mwema na utatatuzi wa migogoro kwa njia ya diplomasia. Kungekuwa au kukiwa na ofisi au kitengo huru cha ubalozi huu Uganda na Rwanda hawangeenda kuutatua mzozo wao kule Angola, mzozo kati ya Rwanda na Burundi ungeshughulikiwa na Jumuiya badala ya kupuuzwa. Lakini hilo ni pendekezo tu.

Hofu ya rasilmali za DRC kuvamiwa na nchi za Jumuiya ni halali lakini haipaswi kuwa. Ni ukweli kuna wale ambao wako na ulafi kwa haya madini lakini idadi yao ni chache kuliko wale ambao watakuwa na mtazamo wa kutoingila na kuvamia rasimali hizo kinyume na mapendeleo ya WanaDRC. Kumbuka maamuzi ya Jumuiya yanafanywa kwa njia ya makubaliano (consensus) kumanisha kuwa inahitaji mmoja anayetofautiana kuweka wengine kiukweli.

Kwa haya na mengi yaliyotajwa awali, Jumuhuri ya ya Kidemokrasia ya Congo wakubaliwe kuingia Jumuiya jana sio leo wala kesho. DRC ni kama msichana mzuri aliyetayari kuenda date lakini ndio sisi hao tunataka kumfanya awe wa kungoja. Anaweza kubadilisha maamuzi yake na akatae kuenda date na Jumuiya kabisa kwa hizo ngoja ngoja. Kwa sababu ya DRC kuwa na strategic importance ya kuunganisha Jumuiya na Bahari ya Atlantic, DRC isikataliwe au kuwekwa pembeni bali wakubaliwe kujiunga na Jumuiya.
 

Mkuu Red Giant unaona kinachoendelea saa siku za hivi karibuni: Kuna mambo mengi ambayo nadhani ni lazima Tanzania na Kenya wakae wayamalize kiuungwana na kindugu. Tanzania ni eneo la muhimu sana ambayo huzalisha chakula kinacholisha maeneo mengi ya Afrika Mashariki: Nadhani hatukutakiwa kuitumia hii nafasi yetu vibaya (Weaponizing Trade) kama silaha ya kisiasa.

Nakumbuka hapo mwanzoni niliwahi kusema kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki haitakiwi ijitanue tena kwasababu ina matatizo lukuki, na moja kati ya hayo matatizo ni Lack of Food Security kama ambavyo imedhihirika siku za hivi karibuni. Kama mwanachama wa jumuiya anaenda kuagiza maelfu ya kilomita kuagiza chakula ambacho kingepatikana kwa jirani yake basi jua kwamba kuna walakini mkubwa sana kimahusiano.
 
Habari wandugu. Inaonekana sasa hakuna tena cha kuzuia DRC kujiunga na ESC. Ujumbe wa EAC upo huko Goma kuangalia kama DRC imekizi vigezo. Na vigezo vikubwa ni.

1. Kupakana na EAC
2.Utayari na uelewa wa viongozi kuhusu haki na wajibu wa member wa EAC
3.Taasisi imara

Kuhusu usalama nimemsikia mjumbe mmoja akisema kuwa anategemea DRC kuwa imara zaidi ndani ya EAC.

Nafikiri sasa inatakiwa tujadili ni jinsi gani watanzania tunaweza kufaidika na ujio wa DRC ndani ya EAC.

Binafsi ntaongea jambo ninaloongea kila siku. Serikali irahisishe upatikanaji wa passport. Urasimu usiwepo. Bei iwe hata 50,000 na pia kigezo cha kupata kiwe kadi ya NIDA tu. Hatuwezi kuzitumia fursa hii vizuri kama hatutarahisisha watu kwenda kuzitumia.
Kwako MALCOM LUMUMBA
 
Hii jumuiya tulikuwa tukikosa nini ambacho sasa tunaweza kukipata kupitia hiyo jumuiya au toka irejeshwe sisi wananchi tumenufaika na nini kutokana na hiyo inayoitwa jumuiya.
 
Usiige kunya kwa tembo utachanika suezi kanali! Tulishindwa EAC ya mataifa matatu je mataifa nane tutaweza? kila raia atakimbilia Tanzania eti kuna usalama na utulivu kisingizio!Bara na visiwani tuu hakieleweki vizuri je nchini somalia utatanua kweli?kumbuka nchi ambazo hazina wakristu duniani ni Somali na saudi arabia.unakumbuka jinsi msomali alivyo waua wakristu pale wategate Kenya? eti kama wewe mkristu anakuua ila muislamu hakuuwi! Hii ni CV ya kuwakatalia kabisaa hawa maadui wa Dini ya emanueli!
 
Moronight walker maoni yangu niliyatoa hapa. Nitakachoshauri leo hii ni kutojihusisha kabisa na hizi siasa za Rwanda, DRC, Kenya na Uganda. Tanzania haiwezi kubadilisha chochote kwenye huu mgogoro.
 
Commented in 2019......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…