Ujamaa ni umasikini na udikteta.Katika kitu ambacho natamani sana ni kuiona Afrika imekuwa nchi moja na kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea hapo ndo itakuwa mwisho wa New world oder plans na tutaizika rasmi. Ingawa naona 2037 inakuja kwa kasi kuliko kasi yetu ya kuziunganisha nchi hizi za Africa. Nitakuwa wa kwanza kwenda kuuzingira mlima Kilimanjaro tuombeane uzima tu. VIVA NYERERE (Mungu akupumzishe kwa amani)
MAGUFULI4LIFE.
Ina maana macho yako hayaoni?Mmeshafaidika na rasilimali zenu wenyewe?
Kwenye hili tunaweza fanikiwa kama tukianza kwanza kuwa na Sera Moja ya Kilimo (Common Agricultural Policy) kama walivyofanya Umoja wa Ulaya mwaka 1962. Nikipata wasaa ntalielezea vizuri hili.Hili suala nimewahi uliza humu, kwanini tusiwe na soko huru la chakula EAC? Tungefaidika sana. Mapinduzi ya kilimo hayaletwi na ruzuku bali soko la uhakika na bei nzuri. Leo EAC kuna soko la watu 168mln. Tumepoteza sana hapa. hatuna sababu ya kujifungia, maana, paradoxically, kufunga mipaka huleta njaa kuliko uhakika wa chakula.
Tatizo bajeti zetu zimetofautiana vipaumbele, sasa unafikiri ni rahisi kuwa na sera moja ya kilimo.Kwenye hili tunaweza fanikiwa kama tukianza kwanza kuwa na Sera Moja ya Kilimo (Common Agricultural Policy) kama walivyofanya Umoja wa Ulaya mwaka 1962. Nikipata wasaa ntalielezea vizuri hili.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yale yale ya Umoja wa Ulaya na Uturuki na Sasa Uturuki imegeuzwa kambi ya kuzuia wakimbizi wasifike Ulaya kwa kulipwa mamilioni ya Euro na kuahidiwa ahadi hewa za kukubaliwa uanachama siku za usoni.Pili, na mwisho kabisa natoa ushauri kama mwanasheria sasa: Congo DRC asiwe mwanachama ila aidha apewe nafasi ya mtazamaji (Observer Status) kwanza ndani ya EAC huku akijifunza mwenendo mzima wa EAC. Sambamba na hilo EAC tunaweza kusaini mkataba maalumu na Congo DRC (Sui-Generis Treaty) ambao utampa nafasi ya kipekee kunufaika kiuchumi bila kuwa mwanachama. Anaweza akaandaliwa vipengele (Extracts Clauses with Limitations ) kutoka mikataba mbalimbali (Protocols) ambayo EAC ameshasaini
Kwanini isiwe rahisi ? Sera ni mwongozo wa kisiasa ambao umeandikwa kitaalamu ili kutimiza malengo fulani ya kimaendeleo kwenye nchi wanachama. Tatizo lako hapa lipo wapi ?Tatizo bajeti zetu zimetofautiana vipaumbele, sasa unafikiri ni rahisi kuwa na sera moja ya kilimo.
Wapi nimeandika kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo awe mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ? Nadhani hujaelewa nilichokiandika hapo au aidha umeninukuu vibaya.Huoni kuwa mwanachama kamili wa EAC ni fursa kwa nchi jirani (zenye makundi ya waasi huko) kuhusika kikamilifu kuimarisha usalama hasa huko Mashariki?
Wakuu mwezi wa 6 mwaka huu DRC iliomba kujiunga na EAC je tuikubalie?. Kwanza tuone hali ilivyo kwenye EAC. Sasa kuna nchi sita, Burundi, Kenya, Tanzania, South Sudan, Rwanda na Uganda. Maombi ya Somalia na DRC yanasubiri kujibiwa. Somali sababu ya usalama na DRC ishu ya Ebola. Lengo kuu la EAC ni kuwa nchi ya mtindo wa federation.
Watu: EAC kwasasa ina watu 168m. Congo ikijiunga tutakuwa watu 259m. Baadaye tukifikia federation tutakuwa wengi kuliko Nigeria, 200m.Wa kwanza Africa na wa Tano duniani.
Eneo: Eneo letu ni km za mraba 2.44m Congo wana 2.345m. Tutakuwa naxeneo la 4.785km za mraba. Wa kwanza Africa na wa saba duniani.
Uchumi: leo uchumi wetu GDP-PPP ni $534bln. Congo wana 77, itakuwa $611bln. Wa tano Africa na 36 duniani. Kwenye GDP-nominal tuna $206bln Congo 46 hiyo $252 Wa nne Africa na 45 duniani, ila per capita yetu itashuka sana. Congo ni chi kubwa yenye rasilimali nyingi sana.
Mnaonaje DRC kujiunga EAC? cc Malcom Lumumba
Mazingira yetu ya kisiasa yametofautiana baina ya nchi na nchi.Kwanini isiwe rahisi ? Sera ni mwongozo wa kisiasa ambao umeandikwa kitaalamu ili kutimiza malengo fulani ya kimaendeleo kwenye nchi wanachama. Tatizo lako hapa lipo wapi ?
Nilikuwa naweka tu facts zisaidie mjadala. ila nna concerns kadhaa. Moja naona kama Congo ikijiunga centre inaweza hamia kigali, maana ndiyoo itakuwa centre ya eneo na mtawanyiko wa watu, ila siyo ishu kubwa. Pia ishu ya mataifa ya kigeni, leo EU wanatupa hela ili tuharakishe EAC. Sidhani kama mataifa ya magharibi yatafurahi Congo kujiunga nasi, maana inaweza fanya iwe stable na kujielewa. Kwenye usalama naamini Congo ndani ya EAC isiyo na blahblah itakuwa salama.
Umeandika asiwe mwanachama kamili ila mimi na mtizamo tofauti yaani kama akiwa mwanachama kamili ndio uwezekano wa hizo nchi jirani kuhusika kudumisha usalama huko Drc Mashariki utapanuka zaidi kuliko Sasa.Wapi nimeandika kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo awe mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ? Nadhani hujaelewa nilichokiandika hapo au aidha umeninukuu vibaya.
Ujamaa ni umasikini na udikteta.
Afrika tuachane na ujamaa tukumbatie ubepari.
Ndio suluhu ya matatizo yetu.
Mazingira ya kisiasa ya nchi zote duniani hayako sawa, hata yale ya nchi zenye viwanda duniani za G7 zimetofautiana lakini kuna baadhi ya mambo wamekubaliana.Mazingira yetu ya kisiasa yametofautiana baina ya nchi na nchi.
Utekelezaji wa hizo sera utategemea zaidi utashi wa kisiasa wa mtawala ndani ya nchi husika, je kama uongozi ukibadilika na mtawala mpya asizipende?
Hapa sijakuelewa vizuri, hebu elezea zaidi.Umeandika asiwe mwanachama kamili ila mimi na mtizamo tofauti yaani kama akiwa mwanachama kamili ndio uwezekano wa hizo nchi jirani kuhusika kudumisha usalama huko Drc Mashariki utapanuka zaidi kuliko Sasa.
Hizi nchi za Rwanda na Uganda (wanachama wa EAC) zimekuwa zikitajwa kuhusika na mzozo wa huko Mashariki mwa Drc kwa muda sasa na pia kuna makundi ya waasi kutoka hizo nchi yanayoendesha Vita huko Drc.Hapa sijakuelewa vizuri, hebu elezea zaidi.
Rwanda na Burundi wako ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini migogoro yao imetushinda Tanzania, Kenya na Uganda mpaka leo. Imetuletea gharama kubwa na upotezaji mwingi wa muda na rasilimali, unadhani Kongo ambayo ni nchi kubwa ndiyo tutaiweza ?Hizi nchi za Rwanda na Uganda (wanachama wa EAC) zimekuwa zikitajwa kuhusika na mzozo wa huko Mashariki mwa Drc kwa muda sasa na pia kuna makundi ya waasi kutoka hizo nchi yanayoendesha Vita huko Drc.
Kama Drc itakuwa mwanachama kamili wa EAC ina maana ni rahisi zaidi kwa hizi nchi kujitolea zaidi kushiriki kumaliza mzozo huko mashariki mwa Drc na zile shutuma za wao kuhusishwa na huo mgogoro zitapungua au kukosa nguvu.