kabingo
Senior Member
- Oct 16, 2015
- 115
- 118
Binafsi naomba tamko la mkuu wa nchii hii kuhusu hii mifuko ya hifadhi ya jamii maana sasa imekuwa ni taabu tupu.
Mara ya kwanza NSSF mlikubali mwanachama anaweza kufungua madai ya kujitoa baada ya kumaliza miezi sita baada ya kuachishwa au kufukuzwa kazi, pamoja na hayo mwanachama alipewa miezi miwili tena ya kuhakikiwa wenyewe wanasema ni kumchunguza mwanachama,ukijumlisha na miezi sita inakuwa miezi nane.
Hivi kweli kama sio kutaka kujineemesha kwa pesa ya wanachama ni nini? Kituko wamekuja na kali ya mwaka mpya, NSSF nadiriki kusema huu mpango mliokuja nao ni wizi wa mchana,
Nakumbuka mwezi wa kumi namoja mwaka jana nilikwenda kufungua madai ya mafao yangu baada ya kumaliza miezi sita tena nikajiongezea miezi mitatu nikaambiwa nirudi mwezi wa kwanza nimekwenda leo nikaambiwa wameongeza mda wa uchunguzi miezi miwili haitoshi niache jina na namba ya simu watanipigia wakishajiridhisha kuwa sijapata kazi tena, nikawauliza uchunguzi wenu unatumia mda gani?
Yule dada wa huduma kwa wateja akasema hawajajua ni kwa mda gani.Naomba wadau tujiulize ndo ile ya kuchukua mafao hadi miaka sitini au inakuwaje. Mkuu wa kaya pamoja na mkuu washirika tunaomba majibu.