Tuijadili Hii Kauli Tata!!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,888
Reaction score
29,690
Habari za mapumziko wana-MMU,.

Naomba Tujadili Kwa Mapana Yake Hii Kauli Ambayo Nimekuwa Nikiiskia Mara Kwa Mara Mtu Anatokea Na Kukuambia ''You Are In Wrong Relationship Au Kwa Kiswahili '' Hauopo Katika Mahusiano Sahihi'',.

Nawakaribisha Tushiriki Kwa Pamoja Kupata Maana Halisi Ya Huu Msemo Unaoshika Kasi Sana!!
 
kwa upande wangu nadhani maana halisi ya maneno hayo ni pale ambapo mmoja wapo katika mapenzi ni kama vile mtumwa au ni kama vile anatumiwa tu au anaonyesha mapenzi zaidi kwa mwenzi wake ambaye kwa kweli hata watu wakiangalia wanaona wazi kabisa kuwa mapenzi hayo yakiwekwa kwenye uzani ni lazima upande mmoja utazidiwa tu,au ni pale inapoonekana una mahusiano na mtu ambaye tabia zake zitakutesa au kukusmubua ilhali wewe u mtu mwema na unayestahili uhusiano mzuri na mtu mwenye tabia za kupendeka,ni hayo tu kwa mimi mkuu.
 

kumbe inawezekana watu wa nje ya mahusiano yenu kugundua hili kabla hata ya wapenzi wenyewe kujua?,..
 
Mbona ni kauli iliyowazi kabisa isiyohitaji mjadala wowote.

Jambo la muhimu ni kumuuliza huyo aliyekuambia hivyo, akueleze sababu za kutamka hivyo.
 
Kimfaacho mtu chake!
Nani ameweka viwango sahihi vya mahusiano? Watu wanakuwa kwenye mahusiano kwa sababu tafauti. Ni juu ya mhusika kuamua kama mahusiano ni sahihi ama la!
 
Mkuu nafikiri unapousikia msemo huo ni vema ukautazama kwa kina kwani yawezekana kweli huenda mwenzi wako kuna mengi nyuma ya pazia anayafanya sasa wanashindwa kukupasulia. Au wamemsikia mwenzi wako pengine anasema kinyume na matarajio yao. Pia tukitazama kwa namna nyingine lbd hawapendi tu wewe uwe na huyo uliye nae so wanakudiscourage.

Jambo la msingi uwapo kwenye mahusiano ni kujiamini na kumwamini partner wako kwani maisha ni yenu na si ya watazamaji. Ila kumbuka lisemwalo lipo so uwe mwangalifu.
 
Mbona ni kauli iliyowazi kabisa isiyohitaji mjadala wowote.

Jambo la muhimu ni kumuuliza huyo aliyekuambia hivyo, akueleze sababu za kutamka hivyo.

sijatokea kuambiwa hivyo ila nahitaji kujua wasemao hivyo huwa wanamaanisha nini hasa,..

Kwani wewe unaelewa nini unaposikia kauli kama hiyo,.
 
yeah na mara nyingi anayekuwa ndani ya uhusiano huo haoni mapungufu kama unavyojua mapenzi ni upofu,au yule mtendwa anaumizwa na tabia za mwenzi wake ila hawezi kuchukua hatua mpaka ashtuliwe na wengine kutoka nje.
kumbe inawezekana watu wa nje ya mahusiano yenu kugundua hili kabla hata ya wapenzi wenyewe kujua?,..
 
Hiyo sio kauli tata kiivyo.
Na inakuaje hadi mtu wa nje akuambie hiyo kauli hapo inamaana wew huoni mapungufu ya mwenzio na kama huoni hiko kitu hapo songa mbele usisikilize ya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…