TUICO mkoa wa Lindi ni jipu lililoiva

MYAO WA KASKAZINI

Senior Member
Aug 10, 2015
133
59
Hivi vyama vya wafanyakazi mkoa vya karne hii ni shida sana.

Hiki chama kinachoitwa TUICO mkoa wa Lindi kina katibu wake mmoja hivi..... Badala ya kuwatetea Wafanyakazi anawatetea waajiri.
Kesi ipo mahakamani, ipo kwenye hatua ya usuluhishi lakini yeye ananyanyua simu yake anampigia mwajiri ili aende wazungumze tena bila uwepo wa mteja wake/mfanyakazi.
Baada ya mazungumzo, anampigia simu mfanyakazi na kumwambia mwajiri amesema atakulipa kiasi fulani cha pesa na kumshawishi akubali huku akimtishia kwamba asikubali kesi iende mbele kwa sababu eti mwajiri atatumia hongo kubwa mahakamani ili ashinde.

Mtu huyu sijui ni wa namna gani. Anamkandamiza mwanachama wa chama chake badala ya kumtetea kuhakikisha anapata maslahi yake.

Sasa mfanyakazi amepewa offer mahakamani, ameikataa. Baada ya kuikataa, Katibu anampigia simu anamlazimisha aikubali. Mfanyakazi anaposhikilia msimamo wake kwamba hataki na hakubaliani na hiyo offer, Katibu anamwambia kwamba kwa sababu amekataa kupokea hiyo offer basi chama kinajitoa. Mfffyuuu.

Hivi huyu Katibu wa TUICO mkoa wa Lindi kwanini haondolewi akaletwa mwingine?!!

Huyu ni JIPU..... TUMBUENI HUYU....... Maslahi yake yapo mbele kuliko yale ya wafanyakazi. Hii sijawahi one.
 
Tena anaenda mbali zaidi anamwambia mfanyakazi nimeshamwambia mwajiri wako aweke pesa kwenye account ya TUICO..... Huku Lindi kwa sababu ya kutojua sheria wanyonge tunaonewa sana na huyu katibu
 
Back
Top Bottom