Tuhuma za Rushwa Kamati za Bunge: Zitto ajiuzulu ujumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
620
1,543
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, ameishtumu Kamati ya Huduma za Jamii anayohudumu kuwa kuna baadhi ya Wajumbe hupokea rushwa.

Kutokana na shtuma hizo ameamua kumuandikia spika kumtaka achunguze na kuchukua hatua.

Kauli yake ianapatikana hapa chini;

"Kuna tuhuma za rushwa dhidi ya Kamati mbalimbali za Bunge ikiwemo kamati ninayohudumu. Nimemwandikia Spika Kuomba Uchunguzi juu Ya tuhuma hizo na kwamba achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na vitendo vya rushwa. Nimejiuzulu Ujumbe wa Kamati ili Kutoa Nafasi Ya Uchunguzi Husika."
 
hahahaha yametimia huwa huyu kijana si ana hizi tuhuma za rushwa maea kwa mara

saasa sa hiii kajiuzuli kwa hasira ama kupisha uchunguzi?
 
Bwana Kabwe kama amejificha flani hivi,hebu aliyekaribu nae amwambie afunguke ni suala gani hasa wamekwama kwa sababu ya rushwa. Maana hiyo kamati inamambo lukuki inayohudumu.
 
Ngoja tumsubiri Job Ndugai ana lipi la kutueleza. Yawezekana ni kweli au ni sehemu ya kutafuta umaarufu. Cha msingi iundwe tume huru ili itupatie ukweli wa hili jambo. Kwa Taasisi kubwa kama Bunge inatia aibu sana kwa kutuhumiwa achilia mbali kupatikana kwa tuhuma kama hizi.
 
Kaona kamati haina maslahi, anyway kama kuna rushwa kweli uchunguzi ufanyike (sa sijui nani atamfanyia nani uchunguzi).
 
Back
Top Bottom