Tuhuma za Dawa za Kulevya: Askofu Gwajima aachiwa kutoka polisi

Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,135
48,821
Kutoka CENTRAL POLICE DSM Naambiwa Askofu Josephat Gwajima ameachiwa kutoka Mahabusu muda huu..

Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima ameachiwa na Polisi leo jioni baada ya mahojiano yaliyodumu toka Alhamisi mchana kwenye kituo cha Polisi kati Dar es salaam kufuatia sakata la dawa za kulevya.

Baada ya kuachiwa Askofu huyo aliandika yafuatayo kwenye mitandao yake ya kijamii “FREE AT LAST: Mungu awabariki wote mlioomba kwa ajili ya jambo hili, kesho nitakuwepo kwa ajili ya Ibada ya Jumapili, Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar es Salaam. Mungu awabariki sana nawapenda nawaombea wote mlioomba kwaajili ya hili”
 
Katoka kweli
75f9bb3302b36a2a0532cafb3f04e029.jpg
 
Back
Top Bottom