Tuhuma ndani ya bunge na kunyamazishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhuma ndani ya bunge na kunyamazishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by keulankubha, Sep 1, 2012.

 1. keulankubha

  keulankubha Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu watanzania mimi nina wasiwasi katika mfumo mzima wa bunge letu. kila kukicha wanaibua hoja nzito lakini ufatiliaji wao ni mdogo sana mfano:-
  1. katika sakata la richmond. limezimwa na wamekubali kunyamazishwa. 2. Dowans, haya nimetolea mfano tu na mengine mengi. Nashangaa sana kama kweli wabunge wetu wapo kwaniaba ya kusimamia serikali katika utendaji kazi. Najua kuwa serikali inafanya kazi kulingana na usimamizi na utekelezaji wa kazi yenyewe kulingana na wabunge wetu watakavyo onesha misimamo ya kusimamia na kutekeleza kazi za kujenga taifa.
  Najua wapo ambao wanaonesha jitiada katika kuibua maovu yanayofanyika ndani ya serikali lakini wananyamazishwa na Speaker wabunge, Ili swala la kunyamazishwa wahesimiwa wabunge wazalendo ninaomba tena sana Msikate tamaa msumbue sana spker kwa hoja binafsi. kila kikao katika hoja hizo ni marudio ya zile anazozikalia tuone kama atazikalia milele. mi ninadhani hawezi kuzikalia kama utakuwepo wezekano wa kulejesha hoja zilezile zikianzishwa.
  2. tatizo jingine sisi wananchi tumekuwa mchango mkubwa katika swala la kukumbatia maovu. sasa ni wakati wetu wananchi wapenda maendeleo ya kweli na wasiopenda madudu yanayofanywa na watawala ccm tuwambie kuwa inatosha. wakirudi nyumbani katika majimbo yao tuwafukuzie mbali na kuwazomea ndio watakoma na wajue kuwa watanzania wa sasa ni tofauti na wa mwaka 40 hivi sasa kila mmoja ni muelewa anaye weza kutambua jema na baya.

  nduzu zangu wabunge tumieni nafasi zenu kunusulu taifa letu

  CCM naomba mujue ya kuwa when a man going down the hill, every one will give him a push.
   
Loading...