Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,846
Nina rafiki yangu namuonea huruma sana, maana jamaa anahonga sana, na nimeanza naye kazi pamoja miaka 4 iliyopita, na nilisoma naye chuo kimoja na darasa moja, bahati nzuri baada ya kumaliza nafasi zilitoka serikalini na tukaomba wote, sote tulifaulu interview na tukapangiwa Wilaya moja.
Sasa mwenzangu hadi sasa hajafanya lolote la kimaendeleo yeye pesa zake ni wanawake tu, sote hatujaoa ila jamaa amezidi sana kwa wanawake, simuonei wivu ila amezidi, nimejaribu kumweleza direct na indirect but naona haelewi kabisa.
Mimi mwenzio nimeweza kujenga nyumba kijijini kwetu na sasa namalizia ujenzi wa nyumba yangu huku nilipo maana mkoa wetu umepakana na mkoa niliozaliwa hivyo nimepanga kuisha hapa hapa rasmi.
Mwenzangu naona yupo busy na wasichana hadi huruma, sikatai kuwa na msichana ila fanya hivyo kwa akili na mahesabu maana umri na muda vinaenda sana.
Wazazi wake waliniita na kuniomba nimshauri rafiki yangu angalau aoe but jamaa akasema bado anakula "raha" maana chuoni alijibana sana kusoma sasa ni muda wa ku-enjoy.
Nimeshindwa sijui nifanyeje au nitumie njia gani kumshauri rafiki yangu kwanza, apunguze starehe, halafu ajipange kimaisha angalau anunue kiwanja na ajenge au aoe kwanza.
Nisaidieni namna ya kumshauri huyu jamaa.