Tufungue bongo za wanaohamia CCM! Tuangalie mafile Yao!

Tufungue bongo za wanaohamia CCM! Tuangalie mafile Yao!

Mkuu ni kitu gani cha maana alichoongea MO pale BBC!!
Sasa ww ulitaka aseme alitekwa na Mambojana au Manenepa ndo umwamini?

Hakusema ulichokitaka ndo maana unaona aliongea utumbo wa chura!
 
Labda umemfahamu Yericko juzi.... Pinda mgongo umsome na kumjua Yericko utakuwa mtu huru....
Yericko muwe mnaambiana ukweli kwenye vikao vyenu, intelligence yenu inafanya nini kama c kuokoa chama?

Mnawaangusha wengi!
 
Dogo katishiwa sana maisha, dogo kaonywa kwamba sio raia wa Tanzania, dogo ndugu zake wametishiwa kuna watu walikuwa wanatumwa kutoka adi ofisi ya Rais kiufupi dogo kaenda kuokoa maisha yake ccm.
 
Kuna muhenga mmoja aliwahi kusema "Everything has a price"
Leo tumeona 'dogo' Elias Michael mbunge nje ya Bunge wa Buyungu Kwa tiketi ya CDM ameamua kujiunga na CCM.

Ukisoma between the lines kuna dark side inayowavuta shimoni hawa watu wa jamii hii. Wahamiaji wapo wa Aina 2, kuna wanaoenda Kwa njaa zao kabisaaaa mf ndg Moses Machali mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Kaka yangu Kafulila. Hawa njaa iliwanyoosha hasa na daima hakuna baunsa kwenye njaa. Aina ya pili ni watu kama kina Mtatiro, Mtulia, Dr Molel na mkuu wa wilaya wa Dodoma ndg Patrobas Katambi. Hawa walinunuliwa Kwa bei tofauti tofauti tena kama biashara ya watumwa, kama mnada yani.

How much did the buyer pay? Hii unahitaji ku-dig deep! Mwanasiasa kama Mtatiro was strong and guru katika upinzani na dau lake lilikuwa nono haswaa. Hii yote wanunuzi walikuwa wanatafuta namna nzuri ya kupunguza wapiga kelele nje ya darasa na wamefanikiwa.

Juhudi hizi zimepelekea democrasia kupalalaizi na sasa we have almost a teethless dogs ambao hata ku-organize maandamano hawawezi. Yaani wakitangaza tu maandamano, kubwa la maadui akiunguruma wapinzani huishia kuchungulia madirishani na kuandamania mitandaoni!

Simlaumu dogo Michael Eliah, he had also the price na real mnunuzi kafika bei na kaondoka huku akipewa shati kubwa la kijani kama turubai la Fuso kwenye Passo!
Najua moyoni anaumia kuona amemsaliti Marehemu Kasuku Birago na wana Buyungu ila ndo hivyo, pesa mwanaharamu! Unaweza kukuta CCM wamemuahidi kumrithi Eng Chiza as umri unamuacha na sharti ni awe wa kijani au atakuwa katishiwa beyond the capacity he could hold akaamua Bora asalimishe maisha yake! Serikali ina mkono mrefu na madaraka ni matamu! So, once a threat need containment or elimination!

Nitamatishe Kwa kusema kuwa hata wengi tuliomo humu kila mmoja ana bei yake! Siasa za harakati tuwaachie kina Che Guevara na Fidel Castro!! Ukibananishwa utayeyuka tu!


Mimi nadhani tunatakiwa kama Watanzania na zaidi sana kama viumbe wenye utashi na ufahamu kuchunguza upande wa pili wa shilingi kuhusu sababu ya hizi hamam hama za watu walioaminiwa na kuonekana Imara kwa misimamo yao.

Kumekuwa na hii kasumba ya kuaminishana kwa lazma kwamba mtu mwenye akili timamu na mzalendo wa kweli ni yule anayejiunga na CHADEMA kutoka kokote kule na endapo mtu atatoka CHADEMA kwenda chama kingine chochote, kunakuwa na stori za kwenye kahawa na kelele za hapa na pale ambazo zinalindwa kwa nguvu ya propaganda ili ziaminike kuwa ni kweli. Sikatai; huenda hizi shutuma za kichadema chadema zina misingi ya ukweli lakini pia upande wa pili unanisukuma kudhani kwamba hizi tuhuma ni defence mechanism ya Chadema, ni very weak na haziwezi kuwa na ukweli hata kidogo.

Kwa nini tusiangalie kwa nini watu wanahama kutoka chadema na kuna nini wameshindwa kukivumilia huko ndani? Kwa nini tuendelee kuwaaminisha watu kwamba Mzalendo yeyote anatakiwa kujiunga na CHADEMA na sio kuondoka chadema kwenda kujiunga na chama kingine chochote.

Anayezungumzia bei za binadamu, nadhani lazima atakuwa na exact figures. Atuwekee hapa bei za walioondoka
 
Ukiamua kukana uovu simama ktk kweli, Ni kheri kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti
 
Mi kuna wanaohamia CCM ambao siwalaumu
Mwenyewe ningemia CCM, sio kwamba naipenda CCM, ila kupambana na CCM sasa hivi na kushinda ni impossible, hata kushinda udiwani tu ni shida sana kwa sasa hivi

Wamepiga marufuku siasa, ila wao wanazunguka wakifanya siasa, Ma DC na ma RC ambao ni wana CCM wanafanya siasa na wamepewa madaraka makubwa mno ya kumsweka mtu ndani akitamka kitu tu kitakachomuudhi
Bado wameapa na kutamka hadharani kabisa, mpinzani hata akishinda uchaguzi, asitangazwe

Sasa kupambana na CCM kwa mazingira haya ni sawa na vita ambayo unapambana na adui ambaye yupo kwenye ngome huku wewe upo kwenye uwanja wa wazi, so wewe huwezi kumshambulia ila yeye anakushambulia kiurahisi tu

Sasa ukikubali kwenda kwenye vita ya adui anayelindwa na ngome huku wewe huna hata ngao ni sawa na kujielekeza kwenda kuchinjwa tu

Mbinu mbadala ni kuhamia CCM na kwenda kuwavuruga, kupigana huko huko ndani kudai demokrasia ya kweli na uwanja sawa kwa wote, wakikufukuza potelea mbali ila hata ungekuwa upinzani ungepatwa ba mabaya zaidi
 
Back
Top Bottom