Tufanye nini kuelekea 2015?

Bayana

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Messages
433
Points
0

Bayana

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2012
433 0
Kama kuna jambo ambalo ni dhahiri kwa sasa kwa Tanzania, ni hamu ya watanzania kupata mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi. Lakini pengo kubwa linaloonekana ni kukosekana kwa nguvu na sauti moja ambayo itaungwa mkono na watanzania kutoka makundi yote ya kijamii bila kujali makabila yao, dini zao, rangi zao, jinsia n.k.

Wakati ikionekana ni wazi kuwa CCM ni chama ambacho watanzania wangependa kikae chonjo ili kupisha mabadiliko na kujikarabati upya, hakuna chama cha upinzani ambacho kinawaunganisha watanzania kufikia malengo hayo kwa mujibu wa tofauti zao.
Hii ni kwa sababu ya mapungufu yafuatayo katika vyama vvikubwa vya upinzani hapa Tanzania:

1)CHADEMA
Kwa sasa ndicho chama ambacho kinaonekana kuwa na nguvu kubwa kama chama kikuu cha upinzani.

Hata hivyo kinakabiliwa na shutuma zifuatazo:
i)Ukabila na ukanda
ii)Ukosefu wa maadili kwa watendaji wake wakuu
iii)Kutokuaminiana kati ya viongozi wake wakuu ikidhaniwa kwamba baadhi ni mapandikizi kutoka chama tawala.
iv)Udini
v)Viongozi wakuu akiwemo m/kiti na katibu mkuu kutokuwa na kiwango cha kutosha kielimu. Katibu – Phd ya dini, M/kiti – Form six

1) CUF
Ni chama ambacho ni cha pili cha upinzani baada ya CHADEMA. Hata hivyo kinashutumiwa kwa mambo yafuatayo:
i)Udini
ii)Usultani wa viongozi wakuu kuhodhi madaraka na kutokuwapisha wengine kukamata nafasi kubwa za uongozi
iii)Kuwa na nguvu upande mmoja wa muungano

2) NCCR: Huko mwanzo kilishawahi kuhusishwa na ukanda na ukabila. Hata hivyo kwa sasa madai haya hayasikiki kwa vile nguvu zake zimepungua kama ilivyo TLP.
3)Vyama vingine vilivyobaki vinachukuliwa kama NGOs za kujipatia mapato kwa waliovianzisha.
Hizi shutma iwe zina uhakika au ni za kukisia, tukubali kuwa ni pengo kwa ukombozi wa kweli wa Tanzania na ni ngumu kuziondoa kwa sasa kwa vile jamii imeshagawanywa kwa misingi hiyo.

WAZO:
Ili kukata kiu ya mabadiliko ya watanzania, ni vyema wasomi mbalimbali maarufu wasiohusika na kashfa hizo hapo juu kuungana na kuanzisha chama ambacho kitakubalika na watanzania wote bila vipingamizi vikubwa. Wasomi waliopo katika vyama vingine hapo juu watashirikishwa katika safu zingine za uongozi ikbidi na ikithitika tu hawana kasumba za ubaguzi au shutuma mbaya ambazo zinaweza kuporomosha uungwaji mkono wa vuguvugu hilo.

Tukifika hapo TZ in 2015 kwa mtindo huo nadhani itakuwa ni vifijo na nderemo kwa watanzania! Kinyume chake, tusahau kuingóa CCM madarakani kutokana na advantage ya mgawanyiko kutokana na tofauti tajwa hapo juu.

Tafadhali weka ushabiki wa chama pembeni unapochangia hii thread! Mihemko ikikuzidi, fanya kama vile hujaiona hii thread!
 

Forum statistics

Threads 1,390,142
Members 528,096
Posts 34,043,685
Top