Tufanye kila linalowezekana kumrudisha Magufuli kijijini kwao 2020!

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
Kuna kila ishara Mheshimiwa Rais Magufuli anaielekeza nchi yetu kwenye machafuko na vurugu, kwa hiyo mwakani tufanye kila linalowezekana tumpumzishe, nafasi ya Urais ni kubwa sana kwake jamani anajitutumua basi tu!

Nafikiria lugha za matusi na wito wa vurugu ambazo yeye, Katibu Mkuu wa Chama chake, baadhi ya mawaziri wake, Spika wa Bunge, Msajili wa Vyama vya Siasa, wakuu wake wa mikoa na wilaya, wabunge na polisi wanazozitoa na kuhamasisha raia wapigwe, wavunjwe miguu na "kuwatia mimba" raia wasiowaunga mkono...nikifikiria hivi naogopa sana, nchi yetu haipaswi kuongozwa na mtu wa namna hii!

Ndugu zangu na sisi tuhamasishane tumtoe huyu mtu, watu kama Lissu, Bernard Membe,,Zitto Kabwe, Freeman Mbowe wanapaswa kupewa moyo na kuungwa mkono tumwondoe huyu Rais mhamasisha machafuko..

We have seen enough of him, akwende zake huko!
 
Kuna kila ishara Mheshimiwa Magufuli anaielekeza nchi yetu kwenye machafuko na vurugu, kwa hiyo mwakani tufanye kila linalowezekana tumpumzishe, nafasi ya Urais ni kubwa sana kwake jamani anajitutumua basi tu!

Nafikiria lugha za matusi na wito wa vurugu ambazo yeye, Katibu Mkuu wa Chama chake, baadhi ya mawaziri wake, Spika wa Bunge, Msajili wa Vyama vya Siasa, wakuu wake wa mikoa na wilaya, wabunge na polisi wanazozitoa na kuhamasishana raia wapigwe, wavunjwe miguu na "kuwatia mimba" raia wasiowaunga mkono...nikifikiria hivi naogopa sana, nchi yetu haipaswi kuongozwa na mtu wa namna hii!

Unapoteza muda wako bure
 
Nakubaliana na huu Uzi mkuu ...
..kwa mtu anaefuatilia haya mambo kwa undani kabisa hawez kukubali haya mambo ...n kama mzee anahofu sana ndo maana anapinga sana upinzani na plan yake mpaka kuwapa watu mamlaka ya kuongea bila kufikiri ,kutoa kauli za vitisho kwa RAIA hii haikubaliki ..watafanya wafanyavyo ila mm na Tim yangu hatukubali 2020...lazma ieleweke ....KUA MPINZANI SIO DHAMBI IJULIKANE
 
Mleta mada uko sahihi
Ndani ya miaka mitatu ya utawala wake Trilion 2.4 hazina maelezo zilipopotelea
Wafanyakazi wanaumia, hakuna nyongeza wala kupandishwa mishahara kwa mujibu wa sheria za kazi
KIKOKOTOWO kakiahirisha makusudi mpaka 2023 ili kupisha uchaguzi wa 2020
Wakulima Kachukua korosho zao kinguvu
Wastaafu wanahangaikia mafao, hawapewi pesa zao wakati mwingine miaka nenda rudi.
Kavunjia watu nyumba Kimara-Mbezi, kawatia watu umasikini wa kufa mtu
Hali ya maisha na kifedha ya wananchi ni ngumu mno

Mimi nitawashangaa sana CCM wakimrudisha huyu bwana kugombea kwa tiketi ya chama chao.

Nchi imeshamshinda huyu mzee amebaki na propaganda za SGR na Stieglers gorge
 
Mkuu nakubaiana na wewe kuhusu kumwondoa kiongozi ambaye hafai kwenye madaraka.
Kwa kufanya hivyo tufanye bila kuvunja amani na bila kwenda kinyume na Katiba ya Inchi.
Sanduku la kura ndiyo njia salama na ya amani ya kumwondoa mtu madarakani.
Tukishindwa kwenye sanduku la kura tunasema tumeibiwa kura.
Kiongozi yeyote akitaka kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni lazima awe na timu ya ushindi kuanzia ngazi ya vitongoji.
Haiwezekani ukawa Rais wa Inchi wakati asilimia zaidi ya 90 ya wenyeviti wa Serikali, madiwani na wabunge wa serikali za vijiji/halmashauri mitaa/kata/jimbo ni wa chama kingine.
Lowasa alipoingia upinzani aliongeza sana ushindi katika ngazi za Ubunge/diwani/wenyeviti kwa sababu alikuwa ni kiongozi maarufu na mwenye uwezo wa pesa.
Kama angejaliwa afya njema na akabaki CHADEMA basi CCM wangepata wakati mkugumu katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Leo hii hata Rais aliyeko madarakani sasa Mh. Makufuli angehama CCM na kuingia CHADEMA, tunauhakika kuwa CCM kwa mara ya kwanza ingeondolewa madarakani.
Kwa sasa Vyama vya upinzani ni dhaifu kuliko wakati wowote ule wa siasa za vyama Vingi.
Udhaifu huu si mzuri kwa afya ya Demokrasia Inchini.
Vyama vya upinzani ni watch dog wa chama tawala ili kisiende kinyume na ilani yao iliyowaingiza madarakani na si kupigania kwa hali na mali, kufa na kupona kuchua Dola.
 
Hakika bila kufanya hivyo, tujiandae kwa machafuko makubwa kabisa nchini, ambayo hayajawahi tokea, tangu nchi yetu ipate Uhuru wake, toka kwa mkoloni, mwaka 1961
Maandamano ya ukuta yaliwashinda hayo makubwa ataongoza nani maana Mbowe alishindwa.
 
Back
Top Bottom