Tufani kali yaua watu 8 Afrika Kusini

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Watu 8 wamefariki baada ya kimbunga kikali kugonga mji wa Cape Town, Afrika Kusini; upepo mkali ambao vyombo vya Habari vya Afrika Kusini, vimeutaja kama "mama wa vimbunga vyote".
Miongoni waliokufa ni watu wanne wa familia moja, ambao walifariki baada ya kuteketea pale radi ilipopiga maskani yao.

Maafisa wa serikali wamesema.

Maelfu ya watu wameachwa bila makao.
Taasisi zote za elimu zikiwemo vyuo vikuu vimefungwa, huku paa za nyumba na zikifumuliwa na upepo huo mkali.

Manusura wametafutiwa makao mapya mahala salama.

Kimbunga hicho kinagonga baada ya kumalizika kwa ukame mkali wa karne kulikumba taifa hilo.
b3a0a5b8253b056ed23643051e447142.jpg
274d393b3e33f659aa595ec54eb75b63.jpg
13ad07da0c35f3b48809e129b6436dca.jpg
e07fa26ea188337f2d08e9f81cf21c50.jpg

Chanzo:BBC
 
cape of storm..mother city..cape of good hope..cape stad jana ilikuwa noma.watu hawajaenda kazini na mashuleni pia hii hali iliwahi tokea miaka 35 ya nyuma ni noma.wenyewe wamekimbia mijengo yao ya baharini.
 
Back
Top Bottom