bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,678
Awali ya yote nipende kuwashukuru waanzilishi wa Taifa hili kwa kutupa zawadi ya upendo,Kuheshimiana,Kusaidiana bila kujali Makabila yetu wala Dini zetu kwa sasa naweza kuongeza bila kujali mirengo yetu ya kisiasa kwani kipindi kile tulikua kwenye Siasa za Monoparty.
Hatuna budi kuendelea kulinda tunu hizo tulizoachiwa na Waasisi wetu kwa hali yoyote ile,na mtu yeyote atakayejitokeza na kwenda kinyume na hayo ni sharti akemewe mara moja.
Hatuna budi kukataa Watu wanaotaka kutugawa kwa kwa njia yoyote ile iwe Kidini,makabila yetu na pia Kisiasa huyo hatufai kabisa kwani mwisho wa yote hayo ni Hasira,Chuki,Visasi na hata kuanza kunyimana Chumvi baina ya majirani wakati sio maisha yetu hayo.
Tukikubali kwamba hakuna aliyekamilika tutaishi kwa Amani sana na Pia kuruhusu Misamaha ndani ya Mioyo yetu,Tusibebane kwa Mabaya mtu unambeba mtu miaka na miaka na kumwazia mabaya tunaambiwa Amri kuu kuliko zote ni UPENDO bila upendo itakua ni Ngumu sana katika safari yetu ya Kimaisha hapa duniani.
Pia unapomtendea mwenzako kumbuka kuna leo na kesho na hakuna hata ajuaye sekunde moja ijayo mbele yake,Tukisoma zaidi tunaambiwa tuwe na AMANI na watu wote siku zote.
Kama ni watoto ukiamua kuwabeba Tumboni wabebe wote au kama ukiamua kuwabeba mgongoni pia Wabebe wote bila kujali Mahangaiko yao watoto wengine watakufinya,Wengine watakuvuta nywele zako Usijali ipo siku watakua na watakupenda Sana maana uliwabeba wote sehemu moja.
Niwatakie Jumapili Njema.