Tuendelee kuiamini michezo ya kubashiri..?

Tuendelee kuiamini michezo ya kubashiri..?

mayowela

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,757
Kuanzia mwaka 2015 kumeibuka kwa makampuni mengi ya michezo ya kubashiri hasa upande wa michezo (mpira nk), kuanzia 2016 kwenda 2017 kukaanzishwa michezo mingine ambayo haikuwa upande wa kubashiri michezo ila ni kubashiri namba nakutuma muamala kisha unashinda,

Makampuni haya yamesajiliwa na bodi ya michezo ya kubashiri, yanalipa kodi kwenye mamlaka husika, kwenye mapango waliyopanga, yanalipa mishahara wafanyakazi wanaoratibu mchezo huo,

Makampuni ya kubashiri mpira ni mengi mengi sana na nchini kwetu inaonekana soko ni kubwa sana,
ila haya mengine ni machache ( Boom Pesa, Daka Pesa, Biko, Supa5, Tatu Mzuka, Insta Moja na mengine nimesahau, japo naona Ttaau Mzuka na Supa5 ni kaka na dada)

Swali nalojiulizaga sana kwa kauli nazosikia vijiweni,
Je Ni kweli watu wanashinda..?
Je huwa ni mipango tu washindi wanatengenezwa..?

Je ni kweli watu wanashinda..?
Wengi niwaonao hushinda lfu 5, 10, 50 mpaka laki, kuna wengine huwekwa hadi kwenye matangazo yao na wanajirekodi wao wenyewe washindi kuwa wameshinda milioni au laki 5, japo hawasemi wametumia kiasi gani mpaka kushinda

Je huwa ni mipango tu washindi wanatengenezwa..?
Hili nakaa katikati, kunawashindi wanaopigiwa simu jinsi wanavopokea hutia ukakasi, yaani hawashangazwi na ushindi wa mamilioni hayo wakati baadae ukioneshwa hari zao wanakuwa choka sana, Pili washindi wengi kwa asilimia kadhaa hutokea mkoa mmoja na inaonekana Dar es salaam ndio kunawashindi wengi tofauti na maeneo mengine, sijawahi sikia mshindi katokea Nanjilinji

Lakini kama ni uzushi, why wawekeze kwa kusafiri mpaka eneo husika nakumzawadia mshindi, kama ni wa mkoani, Na kama wanatuhadaa Benki ya NMB nao ni washiriki, kwa sababu ndio washindi hupelekwa kupokea pesa zao, Benki yenyewe humpokea kama mteja mpya nakumshauri jinsi yakutumia pesa.

Kwa gharama mlizokuwa mnazitumia kwenye matangazo ya TV na redio faida ilikuwa kubwa sana kwa sasa naona mzunguko wa kuingiza kutokana na wachezaji utapungua.

Wapo wanaoamini watakuja tusua maisha kwa kushiriki michezo hii, Kila la kheri
 
Kina honks hangars lilikuwepo n nadhani bado lipo shirika LA bahati nasibu taiga,mbona siku hizi halichezeshi michezo hii na kuwaachia watu binafsi?
Wameshindwa wapi?
Kwanini kila jambo serikali wakisimamia wana feli?
Mfano airtel waliingia nchini na kuanza kuitumia mitambo ya Ttcl wakafanikiwa,kwanini serikali ishindwe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom