Tueleweshane tishio la mchele wa plastic

Ata mimi sikujua kama ushafika huku... Ivi mtu anadanganyikaje na mchele feki? Nchi za wenzetu michele yao haina ladha wala harufu ila kwa michele yetu ya Tanzania utakulaje wali hauna ladha wqla harufu?
Mimi ndo maana sipendi michele ya nje kabisa!!! Mwendo wa mchele wa Mbeya...
mkuu nakaribia kuvuna huko mbeya nasubiri oda yako
 
Hizi ishu za mchele pasua kichwa sana.

Sasa wakiuchanganya na halisi inakuwaje,bado hawajaongezapo na mchanga kisha kuupaka mafuta ya kupikia ili ung'ae.

Dah.
 
Salam,

Waungwana nimeona kuna videos na maandiko mbalimbali yakizunguka katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu aina mpya ya mchele iliyoingia sokoni ambayo ni bidhaa inayozalishwa kutokana na plastic. Hapa niwe muwazi zaidi kwamba ninapozungumzia plastic ninamaanisha mifuko almaarufu rambo.

Baadhi ya walaji toka sehemu mbalimbali duniani wameonekana wakifanya majaribio kwa kudundisha kitonge cha wali ambacho kilidunda Kama kitenesi... Badala ya kuchanguka Kama tabia ya wali ilivyo.

Sasa,
Kwa kuangalia mazingira ya kila siku na namna ya utafutaji ya maisha ya mtanzania, Nadhani ninaweza kuwa victim kwenye hili ka mchele wa plastic. Kama sikuwahi kula kwa kutokujua basi nitakula kwa kutokujua siku za usoni.

Msaada,

Je kuna namna ya kitaalamu au ya kienyeji kutambua mchele Kama ni wa plastic au la ukiwa bado upo dukani??? Kwa wajuzi tusaidiane.
*Unaponunua mchele tafadhali chukua kiasi kidogo tia katika kikombe kisha jaza maji, tingisha mchanganyiko wa maji na mchele uone kama mchele una elea ama uko chini ya maji. Kama unaelea basi huo umetengenezwa kwa plastic na haufai kwa matumizi ya binadamu. Unatengezwa China kuwa makini mtumie na mwengine kunusuru afya zao*
 
Back
Top Bottom