Tucta yataka mikataba Tanesco ipitiwe upya

Tucta yataka mikataba Tanesco ipitiwe upya

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,502
Reaction score
911,254
Tucta yataka mikataba Tanesco ipitiwe upya Thursday, 27 January 2011 21:24

Patricia Kimelemeta
SHIRIKISHO la vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limeitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitia upya mikataba ya makampuni yanayozalisha umeme ili kuondoa tatizo la kuingia mikataba mibovu na kampuni hizo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa ongezeko la gharama na mgao wa umeme ambao kwa pamoja unadaiwa kuwaumiza wananchi wa kawaida.

Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus mgaya aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Da es Salaam kwamba Tanesco imekuwa ikibeba mzigo mkubwa kutoka kwenye kampuni hizo, na kusababisha kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

Alisema kutokana na hali hiyo, Bunge lina nafasi kubwa ya kuipitia mikataba hiyo ambayo imekuwa ikisababisha hasara katika suala la uzalishaji wa umeme nchini na kutopata umeme wa uhakika.

“Mikataba mingi ya umeme ni mibovu, hii inatokana na wajanja wachache kuingia mikataba ya kuzalisha umeme kinyume na taratibu za kisheria,”alisema Mgaya. Alisema endapo suala hilo litarudishwa bungeni, linaweza kupatiwa ufumbuzi wa kina ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua waliohusika kuingia kwenye mikataba hiyo.

Alisema kitendo cha kuongeza gharama za umeme na wananchi kupata huduma ya umeme kwa mgao ni dalili kwamba Tanesco wameshindwa kujiendesha yenyewe.

Mgaya alisema Tanesco inazidi kudhoofika kwa sababu ya kubeba mzigo ambayo siyo ya wake na kwamba serikali inapaswa kuliangalia suala hilo ili waweze kuzalisha umeme kwa kiwango cha juu. Wakati huo huo, maandamano ya Tucta yaliyotarajiwa kufanyika Januari 29 mwaka huu yameahirishwa hadi Februari 12 mwaka huu.

Hatua hiyo inatokana na Shirikisho hilo kushindwa kurekebisha mambo muhimu kabla ya kufanyika kwa maandamano hayo. “Tumeahirisha maandamano hadi Februari 12, mwaka huu, lengo ni kusubiri barua ya polisi kwa ajili ya kuomba kibali cha maandamano hayo,”alisema.


 
Code:
SHIRIKISHO la vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limeitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitia upya mikataba ya makampuni yanayozalisha umeme ili kuondoa tatizo la kuingia mikataba mibovu na kampuni hizo.
 
 Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa ongezeko la gharama na mgao wa umeme ambao kwa pamoja unadaiwa kuwaumiza wananchi wa kawaida

Matatizo siyo mikataba mibovu tu ila nia ya wanasiasa wa ngazi ya juu kuivunja mikataba hiyo ili kujenga mazingira ya kuwalipa wenye makampuni hayo faedha lukuki na wao kugawiwa fungu lao baadaye...................
 
Back
Top Bottom