TUCTA wapongeza serikali kunusuru PSPF

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limepongeza hatua zilizochukuliwa za kunusuru Mfuko wa PSPF kwa serikali kulipa madeni yake na wastaafu kuanza kulipwa mafao yao.

Aidha, wamependekeza wafanyakazi wa mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii wasiendelee kujikopesha fedha ambazo hawawezi kuzilipa hivyo kuathiri hali za kifedha za mifuko hiyo.

Hayo yamo katika risala ya Tucta kwa Rais John Magufuli wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kitaifa jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Katika risala hiyo iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya, iliipongeza pia serikali kwa hatua za haraka ilizozichukua kunusuru hali ya kuzorota kwa Mfuko wa NSSF na ingependa kuona mabadiliko ya utawala ili kulinda fedha za wafanyakazi.

Mgaya aliishauri Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) iwe na meno zaidi kusimamia na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima ya mifuko hii.

“Aidha lipo tatizo la uendeshaji wa mifuko hii kwa gharama kubwa ambayo haifanani na nchi yoyote katika Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, utoaji wa mafao tofauti kwa wanachama na wingi wa mifuko hii, inayoshindania wafanyakazi wachache, tunahitaji kuwepo usawa wa mafao kwa mifuko yote, kupungua kwa idadi ya mifuko hii ili gharama za uendeshaji wa mifuko hii ambazo ni kubwa kuliko majirani zetu zisiendelee kuwepo na uboreshwaji wa mafao ya uzeeni ufanyike haraka iwezekanavyo,” alieleza Mgaya.

“Aidha tunapendekeza mifuko ibaki miwili, mmoja wa sekta ya umma na mwingine wa sekta binafsi. “Tuna imani kwamba mifuko hii itaendelea kuchangia mradi wa nyumba za watumishi unaoendeshwa na Watumishi Housing Company ili wafanyakazi wapate nyumba za bei nafuu.”
 
Back
Top Bottom