MGANGA MCHAWI
Senior Member
- Oct 15, 2015
- 199
- 393
Nmejaribu kujiuliza maswali mengi kuhusu kinachoendelea sasa hivi juu ya wafanyakazi wa umma nimebaki sina majibu.bNini lengo la kuanzishwa kwake? Wafanyakazi wa umma sasa hivi wapo ili mradi siku imepita. Mazingira ya kazi yamekua magumu, watu wanafanya kazi kwa uoga sababu vitisho vimezidi. Promotions zimesitshwa kwa uongo wa mwezi mmoja au miwil ila sasa hivi ni zaidi ya miezi 6 kimya.
Uhamisho hakuna anaejua kinachoendelea. Ajira serikalini zimekuwa kitendawili. Hivi hawa TUCTA hawaoni? Nilijaribu kusikiliza hotuba ya kiongozi mpya aliyechaguliwa hivi karibuni hakuna alichoahidi juu ya wafanyakazi zaidi ya kusema atapambana kuhakikisha mali za shirikisho zinarudi. Hakuna wanachosema chochote kuhusu haki za wafanyakazi.
Hivi hawa viongoz si wamechaguliwa au wameteuliwa? Wanaogopa nini kuikemea serikali kuhusu kinachoedelea? Mbona Kenya wenzetu wameweza, sisi tunashindwa nini???