TUCTA: Waichimba 'mkwara' serikali !

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
Eti! Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limesema halitatasita kuchukua hatua zaidi kwa Serikali kama itaendelea kupuuza madai mbalimbali ya wafanyakazi. Alisema hayo jana' Rais wa shirikisho hilo Bw. Omar Juma, na kusisitiza kuwa hivi sasa hawapo tayari kurudi nyuma kwani wamepata uzoefu wa kutosha. Alisema kuwa TUCTA inataka Serikali iongeze mishahara ya wafanyakazi ktk sekta ya umma kwa asilimia 100% ili waweze kumudu gharama za maisha. Pia alisema kuwa wanataka serikali ichukue hatua madhubuti za kuhakikisha mfumuko wa bei unakuwa chini ya 10% kabla ya April 2013. Pia amesema mishahara na marupurupu kwa sekta binafsi yatangazwe kabla ya April 2013 na KUPUNZA KODI YA MAPATO YA AJIRA NA KUFIKIA KIWANGO KISICHOZIDI ASILIMIA 11%. Na amesema kuwa Serikali iweke wazi mikakati ya kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira badala ya kuendeleza porojo za kupeana matumaini. Source by: majira jumatano. My take: Je kweli TUCTA ina nia ya dhati na madhubuti kuwa tetea na kuwasaidia wafanyakazi watanzania ambao wamekuwa wakikandamizwa kwa muda mrefu miaka nenda rudi? au nao ni porojo tu?
 
Tucta ni wanafiki sana, hawana jipya. Serikali imeshafulia hivyo ukichanganya na unafiki wao kutekelezwa maslahi kama wanavyotaka ni ndoto za Abnuwas.

Kwanza wahakikishe serikali inawalipa mishahara watumishi wake kabla ya X - Mas ili angalau wale vizuri, hiyo ni kama dondoo tu ya nini kipo na kinakuja.
 
..., kwa maana hiyo ule usemi wa kwamba TUCTA ni kama mbwa hasiye kuwa na meno... kazi yake ni kubweka tu, au ni kweli kama tulivyozoea kuwa ndani shirikisho hilo kuna vibaraka wa serikali?
 
Viongozi wa nyama vya wafanyakazi Tanzania hawana tofauti na nyoka wa kibisa au jogoo wa kuchorwa. Porojo 2 cku zinakwenda hamna lolote la maana.

Walimu walipandishwa munkari mwishowe ikawagarimu, waliondolewa kwenye sensa, kwa nini wasije na majawabu badala ya hizo propaganda..tutafanya hivi..vile mwisho wa cku kimya.
 
Tucta, maneno basi, serikali hii haiwezi kuwasilikiza aslani. Tunataka mfanye vitendo na si porojo. Acha porojo tumewachoka. We are sick and tired of you
 
TUCTA ni MAGAMBA wa kufa mtu. ndo maana hawatendi kazi yao ipasavyo kuwatetea wanaodai kuwatumikia. hawa ni ma PUPPET wa CCM hatudanganyiki ng'o
 
..,TUCTA na mimi nina wasiwasi nao. Inaoneka kama wanakwenda sambamba na serikali ya ccm' mara nyingi wamekuwa wakiwaita waandishi wa habari na kuwaeleza uongo na kweli: mara tarehe fulani mgomo nchi nzima, mara tunakwenda kuongea na serikali, mara bado tuko kwenye majadiliano huku siku zinakwenda. Sasa hivi wamesama mwezi April na huku wakisema bajeti hijayo 2013/14 kwamaana mwaka mpya wa fedha. Kweli "fumbo mfumbie mjinga..." na wajinga ndiyo waliwaliwao..., hapa ni kiini macho ili muda uzidi kusonga.
 
TUCTA,Tumechoka na porojo zenu za kijinga,jana mlikuja na hili,leo hili na kesho jingine tena,hamna msimamo,na hao viongozi wenu wachunguzeni kwa makini sana,wamepandikizwa na Serikali,la sivyo mtaendelea kupiga Jalamba na vimishahara vyenu vya kununulia Unga Robo kilo,Amkeni acheni kuburuzwa.
 

mkuu hawa walimu afadhali wangeandamana na kugoma tukajua wamegoma waziwazi sasa wamegoma kimyakimya ni mbaya kama uamini subiri matokeo ya mitihani mwaka huu ni aibu. wasiojua kusoma form one watakua kibao.
 
each and every sector including TUCTA they are under MAGAMBA control, so don ever expect any change at all(same old story-SOS)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…