BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,005
* Hatma yasubiri maamuzi ya Waziri wa Utumishi
Na Dunstan Bahai
Tuesday, 11 May 2010
MAZUNGUZO yaliyokuwa yanasubiriwa kuamua hatma ya mdai ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na serikali Jumamosi hayakuzaa matunda kwani kila upande umeendelea kubaki na msimamo wake.
Mazungumzo hayo ndiyo yalikuwa yanasubiriwa na wafanyakazi ili kujua hatma yao, huku rais huyo akiwa tayari ameweka bayana kuwa serikali yake haina uwezo wa kulipa kima cha chini wanachotaka.
Madai ya msingi ya wafanyakazi hao mbali na kima cha chini cha sh. 315,000, wanataka kupunguzwa kwa kodi kubwa inayotozwa kwenye mishahara kutoka asilimia 15 hadi 9 na marekebisho ya mafao mifuko ya pensheni.
Akizungumza jana, Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA, Bw. Nicholaus Mgaya alisema majadiliano hayo hayakufikia muafaka.
"Kila upande umemaliza mazungumzo hayo ukiwa na msimamo wake. Tumekubaliana kutokubaliana. Mapendekezo hayo ya kila upande yatapelekwa kwa Waziri mwenye dhamana ya utumishi na yeye atatoa maamuzi yake ndani ya siku 21 kuanzia siku mapendekezo hayo yalipotiwa saini na pande zote mbili," alisema.
Bw. Mgaya alisema maamuzi atakayoyatoa Waziri Hawa Ghasia, ni ama akubaliane na upande wa serikali au wa wafanyakazi au asikubaliane na upande wowote na hivyo kuyarudisha mapendekezo yake kwenye meza ya mazungumzo.
Wakati wakisubiri maamuzi ya waziri, Baraza Kuu la TUCTA litakutana mwishoni mwa mwezi huu kuyajadili.
Alisema Baraza hilo kwa kuwa ndilo lililotangaza mgomo, ndilo litakalotangaza tena kuwepo au kutokuwepo kwake.
TUCTA waliandaa mgomo wa wafanyakazi nchi nzima Mei 5, mwaka huu lakini wakiwa kwenye maandalizi ya mgomo huo, siku mbili kabla, Rais Kikwete alitumia nafasi ya kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam kuuzima na kuwatupia lawama viongozi wa shirikisho hilo kwa uongo na unafiki, tuhuma ambazo zimepingwa na kudaiwa kuwa kiongozi huyo amepotoshwa.
Katika hotuba yake Rais alisema serikali haina uwezo wa kulipa kima hicho cha chini kilichopendekezwa na TUCTA na kwamba kutokana na hali ya uchumi hata wakigoma miaka minane, serikali haitaweza kuwalipa na kwamba wakiendelea na msimamo wao huo serikali iko tayari kuwafukuza kazi wafanyakazi wote.
Hata hivyo, TUCTA walisema kauli ya Rais katika mkutano huo ililenga kuwadhalilisha na kwamba hana mamlaka kisheria ya kuzima mgomo huo bali Mahakama Kuu kitengo cha kazi pekee.