Tucta: Serikali imeshindwa kuwatengenezea vijana ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tucta: Serikali imeshindwa kuwatengenezea vijana ajira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 9, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta)  Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), limesema nafasi nyingi za ajira zilizotengenezwa na Serikali kwa vijana ni za kuuza pipi na bidhaa za mikononi barabarani.
  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wake wa Uchumi na Utafiti , John Gonza wakati akizungumza kwenye mkutano uliojadili kuanzisha Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania (Mkukuta) awamu ya pili. Gonza, alisema vijana wengi wamejiajiri kwa kuuza bidhaa barabarani zikiwemo pipi, hatua ambayo haiwezi kuwakwamua kutoka katika umaskini.
  Alisema Serikali kupitia Mkukuta awamu ya kwanza, ilishindwa kutoa majibu ya uhakika kuhusu suala la ajira kwa watu wake na badala yake imeendelea kupanga mipango isiyotekelezeka.
  Aliitaka Serikali kueleza ajira milioni moja ilizotengeneza zipo mikoa gani na katika maeneo yapi badala ya kuzungumzia suala hilo. Gonza, alisema maisha ya wananchi wa kawaida wakiwemo wafanyakazi bado yanazidi kuwa magumu ingawa Serikali inatoa takwimu kuwa uchumi wa nchi unakua.
  Mkurugenzi huyo, alisema takwimu za kwenye vitabu kwamba uchumi wa nchi unakua hazitamsaidia mwananchi wa kawaida kupiga hatua katika maisha yake.
  " Kila siku tunaambiwa uchumi unakua kwa asilimia sita, lakini mbona ukuaji huo hauendani na kubadilishwa kwa maisha ya watu wanaokabiliwa na umaskini wa kutupa ?" Alihoji.
  Akizungumzia Mkukuta awamu ya pili, Gunza, alisema mpango huo ujikite katika kutoa majibu juu ya umaskini unaowakabili Watanzania na kuacha kuwaeleza tafiti za kwenye makaratasi na makabrasha.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirikisho la Asasi zisizokuwa za Serikali, John Ulanga, alisema mashirika 1,600 yalishiriki katika kuandaa mpango huo mikoani kuanzia ngazi ya chini.
  Vilevile, alisema watu 600 nao walishiriki kwa kutoa maoni yao ambayo yatasaidia kuandaa Mkukuta awamu ya pili kwa faida ya wananchi wote.
  Ulanga, alishauri Mkukuta awamu ya pili kukazania mpango wa Kilimo Kwanza kwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wamejiari katika sekta ya kilimo. Akizungumza katika mkutano huo uliowashirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Kijja, alithibitisha kuwa ukuaji wa uchumi bado haujamsaidia mwananchi wa kawaida kujikomboa kutoka katika lindi la umasikini. Kijja, alisema kukua kwa uchumi lazima kuendane na wananchi kuboresha maisha yao na kuwafanya waondokane na umasikini unaowakabili.
  Alisema umaskini unachangiwa na ukosefu wa nishati, miundombinu na nyenzo za kulimia hasa katika maeneo ya vijijini ambako serikali imejipanga ili kulimaliza kupitia Mkukuta awamu ya pili.
  Mkutano huo uliwashirikisha wananchi wa kawaida, walemavu, mashirika yasiyokuwa ya Serikali, wahisani, wanafunzi wa shule za sekondari na viongozi wa serikali.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...