TUCTA mpo kimya kuelekea Mei Mosi

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,502
12,827
Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi mwaka 2020 yamefutwa na Serikali kutokana na Mapambano ya COVID 19. Zikiwa Zimesalia siku 5 kufikia siku hii muhimu kwa wafanyakazi kote nchini sioni hatua wala jitihada zozote za Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi kutetea Maslahi mapana ya Wanachama wao.

Nasema Mungu anawaona nyie viongozi, hivi mmeshindwa hata kuchukua bajeti mliyokuwa mnanunulia FULANA ZA MAADHIMISHO kila mwaka mkawanunulia wanachama wenu Sanitizer japo 500Mls na barakoa angalau 5 kwa ajili ya kujikinga na Covid mahala pa Kazi? Hakika kufa kufaaana, kumbe hamthamini Maisha ya Wanachama wenu kiasi hiki? Au ndio uwezo wenu wa kufikiri umeishia kujilipa Mishahara mikubwa na posho za ujanjau ujanja.

Chama kama CWT angalau wao wana BENKI, Majengo nchi nzima nk, lakini vyama kama TUGHE, TALGWU nk nk nk mjitafakari sana. Tunataka kuona msaada kwa watumishi wenu kwenye janga hili, au hamsikii wauguzi kukosa vitendea kazi? Mmetulia tulii!

Ole wenu wengine sie sio Wanachama wenu mmgerudisha michango yetu.

Weekend njema wadau
 
Back
Top Bottom