TUCTA inatutenga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUCTA inatutenga!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hmaster, Oct 4, 2011.

 1. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wooote wana jf wenzangu. Nawaomba sana mnivumilie kwa kuiweka mada hii katika jukwaa hili kwani naamini jukwaa hili ndilo linalopitiwa na wengi zaidi kuliko mengine hivyo nategemea michango mingi pia.Mimi ni mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu tu katika sekta binafsi hapa nchini na kwamba sijawahi kuajiliwa na serikali tangu nianze kufanya kazi. Katika kufanya kwangu kazi huku nimeshawahi katika nyakati tofauti kujiunga na vyama vya wafanyakazi sehemu za kazi na kukatwa mshahara wangu kwa ajili ya kuvichangia vyama hivi ili viweze kutetea maslahi yetu na haki zetu makazini. Jambo ambalo limenisukuma kuandika mada hii na kuwaletea ndugu zangu ni kuhusu uwajibikazi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA) ambalo hupokea sehemu ya michango yangu kupitia chama changu cha wafanyakazi. Taasisi hii tangu zamani sana ikiwa na majina tofauti katika nyakati tofauti imekuwa ikiwatetea, kuwasemea na kusimamia sana maslahi na haki za wafanyakazi wa serikali kuliko wale tulio katika sekta binafsi. Ukikuta wanalalamika kuwa mishahara ya kima cha chini iongezwe, huwa wanazungumzia ile ya wafanyakazi wa serikali: sasa sisi tulio katika sekta binafsi tutatetewa na taasisi gani? Mbaya zaidi michango yetu wanachukua. Lakini ikumbukwe kwamba wafanyakazi wa sekta binafsi ni wengi zaidi ya wale wa serikali ambayo ina takribani wafanyakazi 300,000 nchi nzima namba ambayo hata jk hakutishika nayo pale aliposema kwamba haitaji kura zao kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Kwa hali hii nani atatukomboa? Matajiri na wanatunyanyasa wanavyotaka na hatuna cha kufanya, maisha yetu yatakuaje? HEBU SOMA TAMKO HILI TENA LA TUCTA KUTOKA GAZETI LA MWANANCHI LEO!Tucta yajipanga kudai nyongeza mishahara kwa uhakika Nora DamianSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (Tucta), linafanya utafiti ili kuishawishi Serikali kupandisha kima cha chini cha mishahara kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.Tucta imesema licha ya Serikali kutofanyia kazi ipasavyo utafiti wao wa mwaka 2006 uliopendekeza kima cha chini kuwa 315,000, wamejipanga kuzungumza upya na Serikali na waajiri na kwamba mazungumzo yasipofanikiwa ikibidi watachukua hatua ngumu.Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kuwapongeza viongozi mbalimbali wa shirikisho hilo, Katibu Mkuu, Nicholas Mgaya alisema utafiti huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.Alisema kwa hali ilivyo sasa utafiti huo unaweza ukapendekeza kima cha chini kuwa Sh500,000 kwani gharama za maisha zimekuwa zikipanda siku hadi siku.“Kipindi hiki ni cha kujitoa mhanga kwa sababu tuna matatizo mengi ya wafanyakazi na mengine tumekuwa tukiyapigia kelele bila mafanikio,” alisema Mgaya.Mgaya alisema kutokusanywa kodi vizuri, ufujaji wa pesa na matumizi mabaya ya Serikali vimesababisha wafanyakazi kushindwa kulipwa vizuri kwa kile kinachoelezwa kuwa ni ukosefu wa pesa.Kwa mujibu wa Mgaya fedha nyingi za Serikali zimekuwa zikitumika kulipana posho kama bajeti ya mwaka 2011/12 ambayo inaonyesha Sh987 bilioni zimetengwa kwa ajili ya posho na bajeti ya mwaka 2006/07 ambapo Sh116 bilioni zilitengwa kwa ajili ya posho.“Mfano Waziri anapokwenda kufungua mhadhara tu analipwa posho Sh1.2 milioni kwa hotuba aliyoisoma kwa dakika 15,”alisema.Katibu Mkuu huyo wa Tucta alisema kama matumizi ya Serikali yakidhibitiwa moja ya maeneo yanayoweza kuboreshwa ni suala la mishahara ya watumishi wa umma.Alisema pia kodi ya mapato na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) bado wanaiona ni kero na kwamba wanaitaka Serikali ipunguze ili iwe chini ya asilimia 10.Kwa mujibu wa Mgaya watu wanaolipa kodi nchini ni milioni 1.5 kati ya Watanzania milioni 40 wakati Kenya yenye watu milioni 38 wanaolipa kodi ni milioni 10.“Wigo wa kodi upanuliwe ili watu wengi walipe kodi na kuwapunguzia mzigo wafanyakazi,” alisema.Shirikisho hilo pia limependekeza kuangaliwa upya kwa mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuondoa tofauti zilizomo kwenye ulipwaji wa mafao baina ya mfuko mmoja hadi mwingine.Kwa mujibu wa Tucta, kero ya utofauti katika mafao ya kustaafu lazima ushughulikiwe haraka kwani wapo wanaolipwa fedha nyingi kwenye mifuko mingine wakati mingine inalipa kiduchu kwa wanachama wanaostaafu.Alitoa mfano kwamba baadhi ya wafanyakazi waliofanya kazi kwa miaka 30 na walipostaafu walilipwa Sh10 milioni katika mfuko mmoja wakati wenzao walioanza nao kazi na kufanya kazi kwa miaka hiyohiyo walilipwa kwa zaidi ya Sh100 milioni
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Thread yenyewe inatia uvivu kuisoma! Labda tuangalie hiyo avatar
   
 3. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mkuu, TUCTA yenyewe imekaa kama chama cha kinyemela vile.. Juzi juzi tu nilisikia walifanya uchaguzi. Hakuna kitu kimeandikwa kwenye magazeti, wala TV... Hapa nilipo hata sina habari ni viongozi gani wamechaguliwa.

  Hivi unategemea chama kama hiki kutetea maslahi yako? Nionavyo mimi, TUCTA ipo kwa ajili ya kutetea maslahi binafsi.
   
Loading...