TUCTA Ifutwe hawawatendei haki watumishi.

afsa

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
1,986
1,585
Rais kwa kutumia katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania nakuomba uifute TUCTA.
Kuna mambo mengi hadi sasa tangu awamu yako ya tano ianze yanayostahili kusemewa na TUCTA wako kimya, hawasemi, wafutilie mbali.

1. Watumishi umewazuia kuhama kwa muda usiojulikana wapo kimya.

2. Marekebisho ya madaraja na kupanda vyeo umezuia kwa muda usiojulikana wapo kimya.

3. Mishahara mipya haijarekebishwa hadi sasa wapo kimya.

4. Haki nyingi za watumishi zinabinywa wapo kimya.

Mheshimiwa Rais nakuomba uifute TUCTA, watumishi hatuoni faida ya TUCTA.
 
Upo Sahihi Mleta Post, Mfano Hapo Pa Kuhamaa, Nashangaa Mtu Kapata Mtu Wa Kubadilishana Ila Mwaka Unakwisha Majina Hayatoki, Familia Tunaona Mara Moja Kwa Mwaka, Hii Tucta Hawasemi Kitu!
 
Upo Sahihi Mleta Post, Mfano Hapo Pa Kuhamaa, Nashangaa Mtu Kapata Mtu Wa Kubadilishana Ila Mwaka Unakwisha Majina Hayatoki, Familia Tunaona Mara Moja Kwa Mwaka, Hii Tucta Hawasemi Kitu!
Hii ya kuhama inawaumiza wengi, hawaelewi wafanye nini huku walipo walishaaga kule waendako hawajapokelewa ni taabu tupu
 
Yaaani inakera sana tena unakuta mtu anahama mwenyewe bila malipo lakini anazuilowa.mambo gani haya ubabe hadi kwenye utaratibu
 
Na Kuna ndugu wa TUTA anaitwa CWWT ambacho kipo ngazi ya Taifa,Mkoa mpaka Wilaya,walipotangaza kujitosheleza kwa walimu wasanii tumewashiba. Nikawaza kwa structure Yao watajitokeza kwa kupitia uhalisia uliopo na kuonyesha mahitaji kama yapo ambayo naamini yapo ili Sirikalii itoke kukanusha ama iweke sawa kumbukumbu zake na si kuburuza watu. Lakini wapo kimya inahuzunisha
Angalau hao tuta kunaissues kama sita waliziweka mezani wakasema wataanza na hizo likiwepo fao la kujitoa kidogo walionyesha wanaanza na kitu flani

Wasalaam
 
Hii TUCTA ni kama haipo,hasa swala ka madaraja mapya kuna walio pata mshahara mpya,ukarudi wa zamani na uhamisho imekaa kimya.
 
Tucta ni wanachama wenyewe kuamua ni nyie kama ni waoga mnadhani hao Viongozi wenu watafanyaje
 
Tujifunze kuandika logic ,nani aifute TUCTA , na hayo madai unayodai kuwa TUCTA imeyanyamizia nani anapaswa kuyatekeleza? . Hebu soma tena post yako ili uone kama kuna mantiki yoyote.

Usikasilike ni ushauri tu....
 
Back
Top Bottom