Tuchukuliane Udhaifu katika mahusiano.

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,641
11,956
Habari wandugu.

Kuna hili jambo ambalo kwa mtazamo wangu nimeona ni la muhimu kushirikishana kutokana kuwa kwa sasa limeonekana kuwa ni tatizo komavu kwenye jamii zetu.

Tujifunze kuchukuliana udhaifu katika mahusiano.
Nikiwa na maana kwamba usiwe mwepesi wa kumuacha mwenzi wako kwa tatizo alilonalo ambalo kimsingi mngeweza kulitatua na maisha yenu yakaendelea.

Umekutana na MTU ambaye humfahamu. Hujui anaishi vipi, alikulia wapi na ana tabia zipi. Lakini ukavutika kumpenda. Sasa basi usitegemee kumkuta akiwa na ukamilifu unao utaka kwa 100%.

Kuna mada nyingi humu na hata mitaani tunakutana na kesi nyingi tu. MTU anakwambia ameachana na mwenzi wake kwasababu ananuka mdomo, sirini n.k.
Ukimuuliza atakwambia alishindwa namna ya kumwambia.(kwanini?). Kama kweli huyo ni mtu unae mpenda huwezi shindwa kutafuta namna ya kumwambia.

Kama uliweza kumtamkia kipindi kile ambapo ulikuwa humfahamu hadi leo mnekuwa wapenzi sasa kinachokushinda hapa ni nini?
Kuna siri gani nzito sasa kati yenu inayoizidi hiyo?.
Mueleze tu ukweli kwa namna ya kumjali kisha msaidie namna ya kutatua hilo tatizo.
Kumbuka yeye hajui kama anatatizo linalokukwaza, ausipo mwambie wewe yeye atajue, wewe ndio msiri wake na unajukumu la kumjulisha hata yale ya sirini yanayo mhusu.
Tambua mtu yeyote mwenye akili timamu anapoelezwa ukweli hakimbilii kupaniki badala yake atatafakari ulicho mwambie hata kama kilimgusa. Hivyo wewe kumwambia si kosa bali ndo msaada anao uhitaji kwako kwa tatizo ambalo yeye mwenyewe halijui.
Anaposema mwili wake ni Mali yako inaama wewe ndio mtunzaji wa hiyo Mali, na unapogundua tatizo kwenye mali yako hutakiwi kuitupa bali ni kurekebisha tatizo.
Usimuache akiumia bila kuelewa kwanini kaachwa, tujivishe ujasiri ili kulinda mahusiano yetu.

Usikarikie kwa kosa ambalo hata yeye lipo nje ya uwezo wake
Mfano.
Utakuta mwenzi wako hana hamu nda tendo.
Sasa usianze kukasirika, si kila anayekosa hamu basi anamchepuko hapana wakati mwingine hilo ni tatizo tu la kiafya. Unachotakiwa kufanya si kuchepuka au kumuacha bali ni kumsaidia kutafuta ufumbuzi.

Ukimuacha utakuwa umemuonea sana, Tambua kuwa huyo hapo alipo ni mgonjwa, anaumwa huyo,

kaanae mshauriane nini cha kufanya na sio kumlalamikia.

Matatizo haya na mengine yanayo fanana na hayo isiwe sababu ya kuvunja mahusiano wakati kuna uwezekano wa kuyatatua.
Kama ukimchukulia kuwa ni mtu tu wa kupitia sawa mwenyewe utakuwa na maamuzi lakini kama kweli unampenda kwa dhati ya moyo wako basi jivike ujasiri wa kukabiliana na changamoto kama hizo kwasababu huwezi jua kuwa we unataka kumuacha kwasababu ya udhaifu wake.
Je unaujua udhaifu wako yeye anaouvumilia?

Haya ni maaoni yangu tu wandugu kutokana na changamoto nilizoziona.

Samahani kwa Maelezo marefu ambayo labda yanachosha ila lengo ni kutaka kueleweka zaidi.

Ahsante.
 
Mkuu uko sawa..kila mtu ana udhaifu wake katika mapenzi. Ni jukumu la wapenzi wote kuvumiliana,kurekebishana na kushauriana kuhusu udhaifu uliopo
 
Mi siwezii naona aibuuu
Mkuu ni sawa, lakini kama aibu ungeanza kuiona kabla hata hamjasex.

Sasa kuna siri gani usio ijua kwake na yeye unasiri gani kwako?

Mwambie tu ukweli au upo tayari muachane kwasababu tu unaona aibu?
 
Back
Top Bottom