#COVID19 Tuchukue tahadhari: Wimbi jipya la covid19 liko kwa jirani

Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,976
3,631
Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema kuna viashiria vya wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kuingia nchini kutokana na nchi jirani wananchi wake kuzidi kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Juni 19, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mkurugenzi wa kinga wa Wizara ya Afya, Dk Leonard Subi ametoa maagizo kadhaa likiwemo la kuwataka wananchi kuvaa barakoa.

“Wizara inawakumbusha wananchi wote kutopuuza ugonjwa wa Covid-19. Wizara imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa huu katika nchi yetu.”

“Hii ni kutokana na taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu zinazofanywa na wizara na mwingiliano kati ya watu wetu na mataifa mengine,” amesema Dk Subi.

Amesema idadi ya wagonjwa wanaokutwa na vizuri vya corona barani Afrika imeongezeka ndani ya wiki tano mfululizo zikiwemo nchi jirani na Tanzania, “maambukizi yanaongezeka maradufu kuliko ilivyokuwa wimbi la pili.”

Katika maelezo yake amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.
 
20210620_174532.jpg
 
Wananchi wahamasishwe zaidi na zaidi kutojazana kwenye mabasi, matumizi sahihi ya barakoa, maana kuvaa barakoa ni jambo moja na uvaaji sahihi ni jambo jingine
 
Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema kuna viashiria vya wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kuingia nchini kutokana na nchi jirani wananchi wake kuzidi kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Juni 19, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mkurugenzi wa kinga wa Wizara ya Afya, Dk Leonard Subi ametoa maagizo kadhaa likiwemo la kuwataka wananchi kuvaa barakoa.

“Wizara inawakumbusha wananchi wote kutopuuza ugonjwa wa Covid-19. Wizara imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa huu katika nchi yetu.”

“Hii ni kutokana na taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu zinazofanywa na wizara na mwingiliano kati ya watu wetu na mataifa mengine,” amesema Dk Subi.

Amesema idadi ya wagonjwa wanaokutwa na vizuri vya corona barani Afrika imeongezeka ndani ya wiki tano mfululizo zikiwemo nchi jirani na Tanzania, “maambukizi yanaongezeka maradufu kuliko ilivyokuwa wimbi la pili.”

Katika maelezo yake amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.
Upuuzi mtupu, ni ushenzi kutia watu hofu kwa ugonjwa ambao ni wa kawaida kwetu, hayo ni mafua kama mafua mengine, tumekuwa tukiumwa na kupona mafua miaka yote, thisi is no different. Kwanza kuvaa barakoa kuna shusha kinga ya mwili kwa sababu unaukosesha mwili nafasi ya kupata maambukizi na kujijemgea natural immunity. Hawa madalali wa chanjo wanatupeleka wapi jamani, kwani hakuna njia zingine za kupiga pesa huko serikalini?
 
Back
Top Bottom