Tuchukue tahadhari kuepuka madhara

Duuh mi nawaza msongamano na usumbugu utakaojitikeza hasa kwa wakazi wa hapa Dar es salaam.

Kwa hali ilivyo hapo jangwani daraja kama halitakuwa limemalizika kujengwa na mvua zikiwa nyingi utegemee usafiri kuwa kipengele kizito sana kwa wenye magari na abiria wa kawaida.

Msongamano mkubwa unatarajiwa kwenye barabara zote za mjini kati na hapa serkali ijitahidi sana kuboresha huduma za mwendo kasi ili angalau kuwasaidia watu kupata usafiri wa uhakika na kupunguza matumizi ya magari yao binafsi ili kupunguza adha ya msomamano na kukaa barabarani kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…