Tuchangie vyama vyetu na wagombea wetu wamudu kampeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuchangie vyama vyetu na wagombea wetu wamudu kampeni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Takalani Sesame, Sep 22, 2010.

 1. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu,
  Katika pitia pitia zangu kwenye vyombo mbalimbali vya habari pamoja na hapa JF tokea kampeni zimeanza kumekuwa na habari nyingi sana za wagombea wa kambi ya upinzani kujitoa kwenye ugombea kwa sababu mbalimbali lakini mojawapo ikiwa ukosefu wa rasilimali za kutosha kufanyia kampeni ikiwemo rasilimani fedha. Ningependa kuamini kuwa mtu unapoamua kujitosa katika kinyang'anyiro cha ubunge au udiwani kunakuwa na maandalizi kadhaa umekuwa umeyafanya ikiwemo rasilimali za kufanikisha kampeni zako lakini je kama huna hela ndo usigombee nafasi ya uongozi kisa huna hela ya kampeni? Je hii haitupelekei kule kuwa 'ukitaka uongozi lazima kwanza uwe na pesa'! Na kama ndio hivyo basi hatuoni hatari kuwa matajiri pekee ndio wataweza kunyakua nafasi zote za uongozi (ubunge na udiwani) kwa kigezo cha kuwa na uwezo wa kufadhili kampeni zao? Na kama mtu yupo tayari kutoa hela kutoka kwenye biashara zake ili awezeshe kampeni zake hatuoni kuwa anaweza kushawishika kutumia nafsi yake pindi akishachaguliwa kurejesha hela yake?! Anyways, jambo la msing nalotaka kusema hapa ni kuwa, kuna haja ya sisi wananchi kuchangia vyama na wagombea wetu kidogo tulicho nacho kama kweli tunamhitaji atuongoze. Kama kweli mgombea ni chaguo lako jaribu kwa namna uwezavyo kumchangia wewe na hamasisha wengine wenye fikra sawa kumchangia mgombea wenu amudu kampeni zake na asije kujiengua ama kwa kukosa hela ya kampeni au kuhongwa pesa na chama kingine cha siasa ajitoe kwa sababu kampeni zake zimechoka! Ni hili ni muhimu hususani kwa vyama vya upinzani ambavyo aidha havina ruzuku kabisa au vina ruzuku kidogo ambayo haitoshi kugawa na kusimamisha mgombea kila sehemu. Pia kitendo cha kumchangia mgombea kinaonesha wewe mwananchi una commitment kwake (it's also expected utampa kura) na yeye atakuwa na commitment kwako kuthamini kuwa bila nguvu zenu wanachi mliojipigapiga asingepata huo uongozi hivyo ana deni la kutekeleza ahadi zake kwenu. Hii inaweza kuwa kinyume na mtu aliyetumia hela zake mwenyewe, labda huenda akwa na kiburi kuwa bila hizo hela zake alizomwaga labda nyie msingempa kura na hivyo akawa hajisikii kuwiwa nanyi. SHIME WANACHI WENZANGU TUJIPIGE PIGE TUCHANGIE WAGOMBEA NA VYAMA VYETU AMBAVYO TUMEPENDEZWA NA SERA ZAKE NA TUNGEPENDA WASHIKE HATAMU!
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  andika neno "chadema" tuma kwenda 15710. Utakatwa sh.350. Nakushauri utumie mtandao wa zain maana voda wana kazi nyingi.
   
 3. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duh! Kwa nini hao Voda wasiwe-confronted waseme kisa cha watu kushindwa kuchangia kupitia mtandao wao..hususani CHADEMA. Kama ni RA basi na iwekwe wazi kuliko upinzani kuwatumia kwa huduma ya WASP wakati wenyewe hawako interested au wamekatazwa. Mitandao mbona iko mingi bado na watu wana multiple lines. Mi mwneyewe nina laini tatu za simu!
   
Loading...