Tuchangie Katika Hili

paramawe

Senior Member
Apr 13, 2013
150
195
Hivi tumekosa Matajiri hata 5 Tanzania wazalendo wakaonganisha Nguvu ya Pesa na kutengeneza Kampuni 1 ambayo itaweza kuwekeza ktk Usafirishaji wa hii Treni kati ya Airport na city Center, then Wakatoa ajira kwa watanzania na wao kuwa wakigawa Faida? Au Mfuko Mmojawapo wa hifadhi za Jamii umeshindwa hii Kitu? Mabenki ya Kizalendo yameshindwa kufanya hii Project na kuwa Mali ya Watanzania. Mbona tunaaibisha Taifa hili jamani? Km 13 tu hata kwa kuanza na Behewa 5 Tumeshindwa?
 

Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,401
2,000
Mkuu wazo lako zuri sana.Lakini umeanzia mbali sana.

We anza na mfano mdogo utakupa picha halisi.
Hivi kwanini baada ya mradi wa Darts kuanza ndio kampuni ya UDA imefufuka kwa kasi na magari mengi na kukamata routes nyingi.
Je ni kweli Matajiri wa Dar wameshindwa kuunda umoja wa kuendesha Darts,au kwanini UDA iibuke na serikali kulazimisha wamiliki wa Daladala kuanzisha kampuni?

Kuna miradi serikali inaitolea macho,hasa hii yenye maslahi makubwa,sasa hapo kwenye train ya kati ya jiji kwa route hiyo kama wanavyofanya baadhi ya nchi za ulaya na zilizoendelea africa kwa hapa hilo tatizo.

Unajua hawa matajiri huwa hawasemi mipango yao,wao wanapeleka proposal serikali,sasa kama ikikataliwa wao wanakaa kimya.Lakini naamini mambo mengi matajiri wetu wanaweza kufanya.issue tu ni kwamba watu hawapati pa kupiga deal.Na Serikali inahofu kwamba itajikuta haina hata mradi wowote wa maana unaomilikiwa na wao kwa silimia mia.

Serikali hadi itoe kitu basi ujue watu wamekisusia mpaka kikadoda na kutia hasara,hapo ndio wataachiwa matajiri.
We angalia Hotels za Serikali zilivyouzwa bei ya ubuyu baada ya kuona majengo yanaharibika na uendeshaji wa hasara.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom