Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Maana nyumba ya sanaa imeuzwa; na kwenye luninga nimeangalia EATV sijaona kipindi kikionesha ngoma za kiafrika; yaani watoto wetu wanaona aibu kucheza lizombe lakini ukiwawekea Rihanna wataruruka kama kuku maji!
Mkuu enzi zile za Asilia Salam, Tumbuizo Asilia, Mkoa kwa Mkoa hazipo tena...Wale wakongwe wa DDC Kibisa Ngoma Troupe, Muungano Cultural Troupe, JKT, JWTZ siku hizi hawana dili tena hakuna mtu anataka kwenda kuwaangalia maonyesho yao. Kila mtu anataka kwenda kuwaona wazee wa Ngwasuma!!
huko tunakokwenda viongozi wanapopokelewa itabidi waanze kupokelewa na vikundi vya hip hop, n.k yaani hata wao wanaona aibu ya ngoma zao!
Hivi, kati ya mambo yote Rais wetu hufanya na kutoa tuzo hatuna tuzo fulani ambazo tunaweza kuwapa wasanii wetu na kuwatambua kwa mchango wao katika kuendeleza na kudumisha utamaduni wetu? Watu kama Bi. Kidude, Remmy Ongala, au hata kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki kama kina Mbaraka Mwishehe na Marijani Rajabu? Au ndio imetoka tena?
Nafahamu kuna Nishani ya Shaaban Robert;kwanini hii isiwe jina la Tuzo ya Shaaban Robert ambapo wasanii mbalimbali (wasioazidi labda watano kwa mwaka) ambao wametoa mchango mkubwa katika kazi za fasihi na sanaa katika miaka isiyopungua ishirini ya kazi zao.
Isiwe tuzo tu ya maneno tu bali pia iendane na mkono wa Taifa lenye shukrani na ninapendekeza kitita kisipungue shilingi milioni 50 (kama dola elfu 50). Kiasi hiki ukitoa kwa watu watano kwa mwaka tu ni kama dola 250 elfu; ukiweka kiasi hicho kwa mwanga wa VX 8 za Mawaziri wenu utaona ni gari moja tu la Waziri - kwa hiyo hoja ya sisi ni maskini inavunjika kabla haijatolewa! (hapa tunaweza kufikiria hata kuongeza na kufanya iwe sawa na kiasi hicho cha 280 milioni!
Ni lazima tutunze na kuenzi sanaa yetu na wasanii wetu. Tuwaheshimu wale waliotuburudisha na kutufanya tufurahia utanzania na uafrika wetu. Vinginevyo tutakuwa ni taifa lisilo na utamaduni; taifa lisilo na utambulisho. Nyerere alisema vizuri kabisa kuwa athari kubwa zaidi ya ukoloni ni kujengwa fikra kuwa utamaduni wetu ni duni na kila kilicho chetu hakifai kuenziwa!
Naomba kutoa hoja, hasa kwa ndugu yangu Nchimbi.. tuwaenzi wasanii wetu. Ni kwa kufanya hivyo tutajikuta tunaenzi urithi wetu sisi wenyewe. Maana tusipoangalia Ubalozi wa Uingereza utaanzisha tuzo ya kuenzi wasanii wetu na sisi tutaenda kushughudia na kushangialia kuwa wazungu wametuhusudu!
Natoa hoja!
Hivi utamaduni wetu ni wa kujivunuia au nao tuuweke jumba la makumbusho?
Kwani kuna utamaduni uliobaki zaidi ya lugha zetu za asili? Hakuna vyakula vya asili( vyooote tunaunga nyanya), hakuna ngoma za asili( zilizopo zimechakachuliwa sana), hakuna jando wala unyago, uharibifu wa mazingira umemaliza kabisa ujenzi wa nyumba za asili, harusi na sherehe zingine na hata mazishi sio yale ya asili( zamani ulikuwa huchangiwi ili uoe!)
Baadhi ya lugha na makabila ya asili vimeanza kutoweka kwa kasi ya ajabu.