Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,463
- 39,929
Hivi, kati ya mambo yote Rais wetu hufanya na kutoa tuzo hatuna tuzo fulani ambazo tunaweza kuwapa wasanii wetu na kuwatambua kwa mchango wao katika kuendeleza na kudumisha utamaduni wetu? Watu kama Bi. Kidude, Remmy Ongala, au hata kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki kama kina Mbaraka Mwishehe na Marijani Rajabu? Au ndio imetoka tena?
Nafahamu kuna Nishani ya Shaaban Robert;kwanini hii isiwe jina la Tuzo ya Shaaban Robert ambapo wasanii mbalimbali (wasioazidi labda watano kwa mwaka) ambao wametoa mchango mkubwa katika kazi za fasihi na sanaa katika miaka isiyopungua ishirini ya kazi zao.
Isiwe tuzo tu ya maneno tu bali pia iendane na mkono wa Taifa lenye shukrani na ninapendekeza kitita kisipungue shilingi milioni 50 (kama dola elfu 50). Kiasi hiki ukitoa kwa watu watano kwa mwaka tu ni kama dola 250 elfu; ukiweka kiasi hicho kwa mwanga wa VX 8 za Mawaziri wenu utaona ni gari moja tu la Waziri - kwa hiyo hoja ya sisi ni maskini inavunjika kabla haijatolewa! (hapa tunaweza kufikiria hata kuongeza na kufanya iwe sawa na kiasi hicho cha 280 milioni!
Ni lazima tutunze na kuenzi sanaa yetu na wasanii wetu. Tuwaheshimu wale waliotuburudisha na kutufanya tufurahia utanzania na uafrika wetu. Vinginevyo tutakuwa ni taifa lisilo na utamaduni; taifa lisilo na utambulisho. Nyerere alisema vizuri kabisa kuwa athari kubwa zaidi ya ukoloni ni kujengwa fikra kuwa utamaduni wetu ni duni na kila kilicho chetu hakifai kuenziwa!
Naomba kutoa hoja, hasa kwa ndugu yangu Nchimbi.. tuwaenzi wasanii wetu. Ni kwa kufanya hivyo tutajikuta tunaenzi urithi wetu sisi wenyewe. Maana tusipoangalia Ubalozi wa Uingereza utaanzisha tuzo ya kuenzi wasanii wetu na sisi tutaenda kushughudia na kushangialia kuwa wazungu wametuhusudu!
Natoa hoja!