Tuanze kwanza na KATIBA ya tanganyika; KATIBA mpya ya muungano ifuate

shumbi

Senior Member
Feb 29, 2012
178
36
Ni ukweli usiopingika kuwa muungano wetu una mapungufu makubwa japo watawala wetu wanaona kama dhambi mtu kutamka hili, lakini ukweli utabaki palepale. TANGANYIKA kwa muda mrefu imeonekana kama ndio TANZANIA ndio sababu wazanzibari wanalalamika kila kukicha wakifikiri wamemezwa na TANZANIA(wakifikiri ndiyo TANGANYIKA).
Lakini ukweli ni kwamba TANGANYIKA iepuuzwa sana.
kwa mfano;

ZANZIBAR ,
1) Wana majeshi (wanaita vikosi maalum)
2) Zanzibar inatambulika kama nchi na mipaka yake (katiba ya zanzibar)
3) Wana wimbo wao wa Taifa
4) Wana bendera yao
5) Wana serikali (Rais wao, baraza la wawakilishi)
6) Wana KATIBA yao

Katika huu mchakato wa kuunda katiba mpya ya muungano; Tufikirie kwanza kuwa na KATIBA YA TANGANYIKA (TANZANIA BARA), Halafu tuunde katiba mpya ya muungano(kama italazimu) kwa kupitia katiba mpya ya ZANZIBAR (Ipo tayari) na katiba mpya ya TANGANYIKA(haipo kabisa; imepuuzwa kwa muda mrefu) kwa kutekelezwa kwa haya hakika utata juu ya muungano utakwisha; Wazanzibari wataiona TANZANIA yao badala ya kufikiri ndiyo TANGANYIKA.

MUONEKANO WA ZANZIBAR NA MUONEKANO WA TANGANYIKA VIFANANE. ZANZIBAR wanapendelewa sana ndio sababi wanafikiri kuwa huu muungano una lengo baya juu yake (wanafikiri wanapewa danganyatoto).
 
Yakhe mulikua wapi sisi huku muungano hatuutaki wala sisi hatujashawishiwa na mtu viongozi wanapata maslahi ndio maana wanajifanya hawaelewi tudhalilike sisi kwa maslahi yao laaa ilikua zamani kuogopana tunataka jamuhuri ya watu wa Zanzibar kwanza katiba zote huko mutajuana baadae
 
Yaani wazanzibar wanajitahidi kutusaidia tupate katiba yetu lakini hatujalitilia mkazo kwa serikali yetu,labda mchungaji Mtikila tu wengine wamelala.
 
Back
Top Bottom