Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Mwakani nchi ya Kenya inategemea kufanya uchaguzi Mkuu ambao kwa baadhi ya wanasiasa wa nchi hiyo hasa Raila Odinga unaweza kuuita ni uchaguzi wa kufa na kupona, Raila Odinga na wenzake wameshajipanga siajabu klk wakati wowote ule kumuondoa Raisi Uhuru Kenya madarakani aidha kwa njia ya kawaida ya kura au ikishindikana kwa nguvu lkn ni lazima aondoke kulingana na wao wanavyosema!
Hivyo hali inatisha sana nchini humo kwani ikumbukwe kwamba Uhuru Kenya ni Raisi ambaye atakuwa anagombea kupata muhula mwingine baada ya kumalizia huu wa kwanza, hivyo kwa hali ya kawaida ana nafasi kubwa sana ya kushinda lkn siyo kwa tofauti kubwa ya kura yaani ni ngumu sana kama vile sisi CCM ilivyoibwaga ukawa kwa tofauti ya kura milioni 2 ambapo ni karibia asilimia 20% ya kura zote jambo linaoloondoa ubishi wowote ule Duniani hata Mbinguni lkn kwa Kenya hilo ni gumu sana kutokea hivyo ina maana tofauti ya aliyeshinda na aliyeshindwa labda itakuwa 1-2% na hapo ndipo sasa shida itakapo kuja, ikumbukwe kwamba kwa Mwafrika msamiati ya kushindwa haupo kwenye orodha ya misamiati yake kama asemavyo fisadi Lowasa!
Hivyo ningependekeza sisi kama TanZania tuanze kujiandaa kuisadia nchi hiyo pindi ilipukapo, kwani hili liko wazi kabisa ikiwezekana tuimarishe kambi yetu Monduli ili kikiwaka basi tuingie haraka sana Nairobi ili kuweka bufferzone na kuokoa maisha...!